SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, April 29, 2016

JIJI LA DAR ES SALAA KUNUFAIKA NA UPATIKANAJI WA MAJI.

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi, Isack Kamwela akijibu swali la Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam. 
  Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu Dkt. Abdallah Possi akijibu la Stella Ikupa Alex (Viti Maalum) alitaka kujua upatikanaji wa zabuni za kazi kwa watu wenye ulemavu leo Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akifafanua jambo Bungeni leo mjini Dodoma.
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam.
 Silafu Jumbe Maufi (Mbunge Viti Maalum) akiuliza swali leo Bungeni mjini Dodoma alilotaka kujua ni lini Serikali iatamaliza tatizo la upungufu wa vifaa vya kufundishia somo la TEHAMA na walimu wa masomo hayo katika mkoa wa Rukwa.
  Wabunge waliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma. 

 Waziri wa Habari, Utaaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa na Mpiga picha wa Gazeti la Jambo Leo Richard Mwaikenda kabla ya kuingia Bungeni leo  mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla akielekea katika ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge  wa Ilala  Azzan  Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Angeline Mabula bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Ahmed Shabiby wa Gairo (kushoto) na Suleiman Ahmed  Saddiq wa Mvomero, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Butiama , Nimrod Mkono kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI itaendelea kutekeleza ahadi zake ilizoahidi ya kuwapatia maji wananchi wake ikiwemo wakazi wa jiji la Dar es salaam ili kutatua adha ya maji inawakabili katika maenneo yao. 

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mahandisi Isack Kamwela wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Ubungo jijini Dar es salaam Saed Kubenea lenye vipengele (a), (b), na (c) lililohoji ni lini Serikali itamaliza tatizo sugu la maji katika Jiji la Dar es salaam.

Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali imekamilika na kufanikisha upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini na ulazaji wa bomba kubwa lenye kipenyo cha mm 1800 kutoka Ruvu Chini hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 56.

“Hali ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam inaendelea kuimarika kwa kuzingatia kuongzeka kwa uzalishaji maji kutoka Ruvu Chini ambao una uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 za maji kutoka lita milioni 180 za awali kwa siku” alisema Mahandisi Kamwela.  

Katika kuhakikisha jiji hilo linakuwa na maji ya kutosha kwa wakazi wake, Mahandisi Kamwela amesema kuwa mradi wa upanuzi wa Ruvu Juu nao umekamilika na una uwezo wa kutoa maji lita milioni 196 kutoka lita milioni 82 za awali kwa siku.

Ili kuhakikisha maji yanawafikia walengwa, Mahandisi Kamwela kazi za ulazaji za ulazaji wa mabomba mawili kutoka Mlandizi hadi Kimara, ujenzi wa tenki jipya la maji eneo la Kibamba na ukarabati wa matenki ya Kimara zimefikia wastani wa asilimia 98, hatua hiyo imewezesha majaribio ya uendeshaji wa mitambo hiyo kuanza mapema Aprili mwaka huu.

Aidha,  Mahandisi Kamwela amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa Kimbiji na Mpera  ambapo hadi sasa mkandarasi amekamilisha uchimbaji wa visima tisa kati ya visima 20 ambapo kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu, hadi kukamilika visima hivyo vitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 260 kwa siku. 

Hadi sasa uzalishaji wa maji katika jiji hilo umefikia lita milioni 390 kwa siku ikilinganishwa na mahitaji ya lita milioni 450 ya sasa.

Akijibu swali la nyongeza la Kubenea alioitaka kujua maeneo yatakayonufaika na miradi hiyo ya maji, Mhandisi  Kamwela ameyataja maeneo hayo yatakayonufaika ni pamoja na maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani.

Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala kwa upande wa Ruvu Chini wakati Mtambo wa Ruvu Juu utawahakishia wakazi wa maeneo Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata.

Kukamilika kwa miradi yote itaongeza uzalishaji na upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam hadi kufikia lita milioni 750 ambayo yatakidhi mahitaji ya wakazi hao hadi kufikia mwaka 2032.

0 comments:

Post a Comment