SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, February 25, 2016

TIGO YAFIKISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA 4G LTE MOSHI

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (katikati)  akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE jijini Dodoma, kushoto ni Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi na kulia kwake ni Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini  Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.
Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katikati ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata na kulia kwake ni  Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini  Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE jijini Dodoma, kushoto ni Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi na kulia kwake ni Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.

Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katikati ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata na kulia kwake ni Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.

Moshi, Februari 24 2016. Wateja wa Tigo waishio Moshi sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.

‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es Salaam kuanzia mapema mwaka jana,’’ amesema Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini, George Lugata.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Moshi, Lugata amesema: "uzindu wa 4G ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."

Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa urahisi kutoka kwenye mtandao wa intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma hii pia inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao.

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Moshi kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti yenye kasi zaidi,” Lugata amesema. Moshi ni moja wapo ya miji mikubwa Tanzania, na pia inajivunia bandari ndani ya Afrika Mashariki na kwa sababu ya bahari ya Hindi ni kivutio cha utalii nchini.

Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama bonasí.

Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G inapatikana kuwa ni Moshi, Dodoma, Morogoro, Tanga na Arusha, “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufikisha huduma ya 4G katika kila kona za nchi ifikapo mwaka ujao, Lugata ameongeza kusema.

0 comments:

Post a Comment