Mkuu
wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa
Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza waliokaa kushoto) wakati
alipotembelea ofisini hapo. Wengine ni watendaji wa ofisi ya Mkuu wa
Mkoa huo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (waliokaa
kulia).
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla mapema leo Februari 15, ametembelea kambi
ya Wagonjwa wa Kipindupindu pamoja na wale waliokumbwa na mafuriko
katika kijiji Mboliboli Kata Pawaga Wilayani Iringa ambapo hadi sasa
kambi hiyo ina wagonjwa 40 huku zaidi ya wagonjwa 223 walilipotiwa
kuugua tangu kipindupindu kimeanza katika eneo hilo.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza wakati wa kutoa taarifa yake kwa
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aliyetembea ya Mkuu wa mkoa huyo,
alimweleza kuwa kati ya wagonjwa hao 223, wagonjwa 17 ni watoto walio na
umri wa chini ya miaka 5, Mbali na hao hadi sasa yamesababisha kifo
kimoja.
Ugonjwa
huo umeelezwa kuwa umewakumba kutokana na mvua zilizonyesha na kubomoa
vyoo na kutapanya kinyesi hali iliyopelekea ugonjwa huo kusambaa Zaidi
katika makazi ya wananchi hao.
Hadi
sasa eneo hilo limekumbwa na maji huku wananchi wakilazimika kuyakimbia
makazi yao na hata kuzungukwa na maji karibu eneo kubwa na usafiri wa
watoa huduma kuwa wa shida ikiwemo kutumia boti maalum ama chopa.
Mkoa huo ulikumbwa na mvua mnamo Februari 3 hadi leo bado maji yameendelea kuzingira maeneo ya vijiji hivyo.
Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog-Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa taarifa namna ya kamati
yake ilivyopambana usiku na mchana na hatua waliofikia katika kuakikisha
kipindupindu kinakwisha katika eneo hilo huku wakiendelea na jitihada
za kupambana na mafuriko ikiwemo kuokoa wananchi waliobakia eneo hilo.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa mara
baada ya kumaliza kwa mazungumzo na taarifa fupi juu ya ugonjwa wa
kipindupindu kwenye maeneo ya vijiji vya Mkoa huo ambapo hadi leo
wamefikia jumla ya wagonjwa 40.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Iringa, Richard Kasesela wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Nduli,
Iringa tayari kwa kuelekea kupanda Chopa kuelekea kwenye maeneo
yaliyokumbwa na mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
Wakielekea
katika Chopa maalum ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwafikia wananchi
waliozingira na maji ya mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipanda Chopa tayari kuelekea kwenye
eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Pawaga,
Mkoani Iringa.
(Picha zote na Andrew Chale, Iringa).
0 comments:
Post a Comment