Karenzi Karake
Mkuu wa upelelezi nchini
Rwanda,ambaye alikuwa anasakwa nchini Hispania kwa makosa ya uhalifu wa
kivita,sasa amekamatwa mjini London.
Kitengo cha habari cha BBC
cha BBC Newsnight, kimegundua kwamba askari wa kikosi cha Metropolitan
walimkamata Karenzi Karake kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow mnamo
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kikosi hicho cha askari wa
Metropolitan tayari kimethibitisha kwamba Karenzi ambaye sasa ana umri
wa miaka 54, amefikishwa katika mahakama moja ya Westminster baada ya
kuwekwa kizuizini kwa hati ya kukamtwa ya umoja wa ulaya, na atasalia
kizuizini mpaka mwishoni mwa wiki hii.
Karake alikuwa ni
mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa wa Rwanda .Karake alipigana vita vya
wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda mwaka 1990 hadi mwaka 1994 na baadaye
alipata cheo cha kamanda msaidizi wa vikosi vya kulinda Amani vya umoja
wa mataifa huko Darfur. Karake ni miongoni mwa makamanda walioko kwenye
orodha ya makamanda wa Kinyarwanda wapatao 40 ,waliomo katika hati ya
mashitaka iliyotolewa mwaka 2008 na kikosi cha uchunguzi cha Hispania
kinachoongozwa na jaji Andreu Merelles.
Mahakama hiyo ya nchini
Hispania inamtuhumu Karake, kwamba wakati alipokuwa kiongozi mkuu wa
kijeshi wakati wa mauaji ya kimbari, aliamuru mauaji ya watu kadhaa.
Lakini pia kiongozi huyo wa kijeshi anatuhumiwa pia kwa kuamuru mauaji
ya raia watatu wa Hispania waliokuwa wakifanya kazi katika asasi moja
ijulikanayo kama Medicos del Mundo nchini Rwanda.
Kukamatwa kwa Karake kuna uwezekano mkubwa wa kuiingiza serikali ya Uingereza katika mgogoro wa kidiplomasia na nchi ya Rwanda.
Inaarifiwa
kwamba Mnamo mwaka 2013 Rwanda ilikuwa inashika namba 18 miongoni mwa
nchi zinazopokea misaada ya kiwango cha hali ya juu kutoka Uingereza.
Karake
ni wa kwanza kukamatwa miongoni mwa makamanda wa ngazi ya juu wa jeshi
la RPF kwa mashtaka yanayomkabili nje ya nchi yake. Wakili Jordi
Palou-Loverdos, anayewakilisha watu 9 ambao wameuawa wenye asili ya
Hispania ameiambia BBC, "Tunaamini kwa haki ya marehemu ninaowasimamia
itatendeka na haraka Karenzi Karake atapelekwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili na huko atajitetea yeye mwenyewe.
Na tunaamini
kwamba wanasiasa na wengine wenye mvuto na kesi yake hawataingilia kati
na kuizorotesha kesi, haki,ukweli na fidia vitapatikana."
HABARI NA BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment