Picha ya Marehemu John Nyerere aliyefariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.
Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini
Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa Kapteni wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ni
kwamba marehemu amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na
kisukari kwa muda mrefu.
Enzi za uhai wake John alishiriki vita ya kumng'oa Nduli Idd Amini nchini Uganda.
Mungu ailaze roho ya marehemu John mahali pema peponi. AMENI
Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akisaini kitabu cha rambi rambi
nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani jijini Dar es Salaam ambapo alifika
kumpa pole Mama Maria Nyerere na familia yake kufuatia msiba wa mtoto wa
Baba wa Taifa John Nyerere.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Katibu wa
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye walipokutana nyumbani kwa Baba wa Taifa
Msasani jijini Dar es Salaam kuhani msiba wa John Nyerere.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa John Nyerere.
Ndugu akitoa pole kwa Mama Maria Nyerere.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpa mkono wa pole Mama Maria
Nyerere kufuatia msiba wa mtoto wake John Nyerere kilichotokea jana
jijini Dar es salaam.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mama Maria Nyerere
alipofika nyumbani kwake kumpa pole kufuatia msiba wa mtoto wake John
Nyerere, wengine pichani ni Makongoro Nyerere (kushoto), Mwenezi wa CCM
mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi, na Anna Nyerere.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Makongoro Nyerere
Msasani nyumbani kwa Baba wa Taifa wakati wa kuhani msiba wa John
Nyerere.
(Picha zote na Adam Mzee)
0 comments:
Post a Comment