SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 16, 2015

Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Filamu yashauriwa kutangaza Tasnia ya Filamu kimataifa

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akizungumza na wadau wa filamu waliofika katika Ofisi za Wizara hiyo kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini itakayofanyika tarehe 23 Mei mwaka huu. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA Bibi. Caroline Gachara Gul (kulia) akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini kwa Uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na watendaji kutoka Bodi ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo Bibi. Siima Rubibira.
Wajumbe kutoka Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA pamoja na maafisa wanaosimamia Filamu nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini mjumbe aliyekua akichangia (hayupo pichani) wakati wa kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo hizo kwa uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.(Muro)

0 comments:

Post a Comment