========
PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi
wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP)
imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi
iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake.
Mratibu wa Mradi huo ametaja
changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa
waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni
hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo.
Mratibu huyo alizitaja changamoto
hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha
inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa
kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs,
Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza program na changamoto
nyingine katika utekelezaji mradi.
Alisema mradi huo unaofadhiliwa
kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania
tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha
nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma
ili kuleta maendeleo endelevu.
Aidha alisema licha ya changamoto
zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu
ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa
usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa,
kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza
kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo
kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma.
Mradi pia umefanikiwa kuimarisha
ushirikishaji wa utayarishaji wa bajeti kuanzia ngazi za chini, kutumika
kwa mfumo wa SBAS ambao unatoa fursa ya kuingiza mahitaji ya Mpango wa
miaka mitano na kugawa rasilimali na pia kuchapishwa kwa taarifa ya
utekelezaji wa bajeti, ukaguzi mbalimbali hivyo kuongeza kiwango cha
uwazi.
Mengine ni pamoja na kutungwa kwa
sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 badala ya sheria
iliyokuwepo Na. 21 ya 2004. Sheria hii pamoja na mambo mengine imeiweka
PPRA kutoshughulikia masuala ya michakato ya ununuzi, na kubaki na
shughuli yake kuu ya kutoa miongozo ya ununuzi wa umma. Vile vile sheria
imeongeza kiwango cha uwazi zaidi katika michakato ya ununuzi wa umma.
“…Kujenga uwezo wa watumishi
katika kufanya kazi zao zinazohusiana na usimamizi wa fedha za umma. Kwa
mfano mafunzo kadhaa yalitolewa kwa wahasibu, wakaguzi, wachumi;
maafisa wa ununuzi…kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kulitumikia
taifa. Kuandaa na kutoa taarifa za kifedha chini ya mfumo wa IFMS ili
kufikia vigezo vya kimataifa (IPSAS), Kuwekwa kwa mfumo wa kusimamia
mali za serikali (Asset tracking software) katiak ofisi zote za
kurugenzi ya Usimamizi wa Mali za Serikali.” Alisema Mratibu huyo.
Mafanikio mengine ni kuongezeka
kwa uwezo wa NAOT hata kufikia kiwango cha hatua ya 3 ya AFROSAE,
uhuishwaji wa mifumo ya fedha kama EPICOR ili iweze kufanya kazi kwa
ufanisi zaidi (k.m. mfumo wa EPICOR toleo la 7.3.5 ulibadilishwa na
kuingizwa toleo la 9.05 wenye modules nyingi zaidi kuliko ule wa mwanzo,
Kufanyika kwa zoezi la uhamishaji wa fedha kwenda serikali za mitaa na
kuweka Mpango Kazi ili kuboresha uhamishaji wa fedha toka serikali kuu
kwenda kwenye LGAs.
Mratibu alibainisha kwa sasa Ofisi
ndogo za hazina zote nchini zimewekewa mfumo wa IFMS, na hivyo kuongeza
ufanisi, Uandaaji na utoaji wa taarifa ya fedha za serikali kwa kutumia
mfumo wa IFMS na kwa kufuata mifumo ya kimataifa ya International
Public Sector Accounting Standards Cash Basis (IPSAS).
Mradi wa PFMRP ulianzishwa
mwishoni mwa miaka ya 1990, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi,
kuongeza uwazi na uwajibikaji na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika
serikali na taasisi zake, huku ikitekelezwa sambamba na programu
nyingine za kitaifa katika sekta ya umma.
0 comments:
Post a Comment