Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza kwa niaba ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye
ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya
wanyamapori uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige)
Na Mwandishi Wetu
RAIS
Jakaya Kikwete ameitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania
katika kukabiliana na majangili wanaomaliza tembo kwa lengo la kupata
pembe zao.
Alisema kutokana na biashara nzuri ya pembe hiuzo duniani majangili wamekuwa na soko tayari kiasi cha kuendeleza vitendo vyao.
Alisema
mitandao iliyopo inawezesha kuuawa kwa tembo hao na kufikishwa bidhaa
za pembe katika soko haramu ambalo lipo duniani na hivyo bila
ushirikiano wa kimataifa wanyama hao ambao ni urithi wa dunia watatoweka
kabisa katika miaka ijayo.
Amesema takwimu zilizopo sasa nchini za tembo zinatisha.
Alisema
mathalani kwa ujangili pekee kwenye mfumo wa ekolojia wa Selou-Mikumi
tembo waliobaki ni 13,084 kwa mwaka jana kutoka Tembo 109,419
waliokuwepo mwaka 2006.
Alisema
mfumo uliopo wa ujangili na soko la bidhaa hizo unafanya vita
inayoendeshwa na Tanzania kuwa ngumu kama haitapata ushirikiano na
mataifa mengine.
Alisema
kutokana na ukweli huo wanataka mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa
kuingia katika mapambano ya kudhibiti biashara hiyo na hivyo kuwamaliza
majangili na kuendelea kuhifadhi Tembo.
Katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili
na hifadhi endelevu ya wanyamapori, alisema serikali ya Tanzania
imeanzisha mchakato wa kulinda wanyama pori.
Baadhi
ya wadau kutoka nchi mbalimbali wanaohudhiria mkutano huo akiwemo
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa
pili kushoto).
Mchakato huo ni pamoja na kuimarisha doria , kuendesha operesheni za kukabiliana na ujangili.
Alisema
pamoja na kuwapo kwa juhudi za makusudi za kukabiliana na ujangili
serikali ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali
zikiwemo za kifedha na raslimali watu.
Aidha kumekuwepo na ushiriki mdogo kutoka kwa wananchi katika vita dhidi ya ujangili.
Alisema
kutokana na haja ya kukabili ujangili na kuwa na hifadhi endelevu,
Februari mwaka huu mataifa ya Botswana, Chad, Garbon na Ethiopia
yalitiliana saini mkataba wenye lengo la kupunguza mahitaji ya bidhaa za
wanyamapori, kuimarisha sheria zilizopo dhidi ya ujangili na pia
hifadhi na kusaidia maendeleo ya maeneo yanayokabiliwa na changamoto ya
uwindaji haramu.
Rais
Kikwete alisema katika hotuba yake kwamba kuwepo kwa mataifa hayo
katika mkutano huo ni kuendeleza makubalino ya kutojishughulisha na
biashara za bidhaa za wanyamapori kwa miaka 10 au hadi hapo tembo
waliopo bara la Afrika watakapokuwa wameondoka katika hatari ya
kuangamizwa katika uso wa dunia na majangili.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi
endelevu ya wanyamapori uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha kwenye
ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha
rais alisema kwamba mkutano huo wa Arusha unatarajiwa kuona namna ya
kuendelea utekelezaji wa makubaliano ya London, Uingereza ya hifadhi ya
wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka akiwemo Tembo.
Alisema
kutokana na mfumo wa ikolojia na hifadhi ya wanyama na majirani zake,
Tanzania inataka majirani kushiriki katika kulinda na kuhifadhi ikolojia
hiyo na wanyama waliopo na sio kuiachia Tanzania pekee.
Tanzania
ikiwa na eneo la kilomita za mraba 943,000 asilimia 30 ya eneo lake na
15 imetumika kwa hifadhi ya wanyamapori na misitu.
Amesema
eneo hilo hutumiwa zaidi kwa ajili ya utalii wa wanyamapori ambapo
asilimia 17 ya pato la taifa linatokana na utalii huo.
Wakati
huo huo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez ,ameipongeza Tanzania kwa kuitisha kikao cha kujadili ujangili
na uhifadhi endelevu wa misitu.
Mwenyekiti
wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya
wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush
Arha akiwakaribisha wadau wanaoshiriki mkutano huo kutoa maoni yao
katika udhibiti wa ujangili ulioshika kasi.
Akizungumza
kwa niaba ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Kenya na Msumbiji
alisema Umoja wa Mataifa unajisikia furaha kuona mataifa wanachama
yanakabilian na changamoto ya ujangili na uhifadhi wa misitu kwa namna
ambavyo itasaidia kizazi kijacho.
Mratibu huyo alisema kwamba ujangili unatishia maendeleo, mazingira na usalama kitu ambacho Umoja wa Mataifa unakipiga vita.
Anasema
biashara ya bidhaa za wanyamapori zinahatarisha uwepo wa wanyama ambao
tayari wapo katika hatari ya kutoweka, unasababisha rushwa na migogoro
ambayo inahatarisha maihsa ya watu.
Alisema
kwa sasa dunia imekuwa ikipungukiwa na tembo wa Afrika kwa kasi
isiyokubalika kutokana na vitendo vya majangili na hivyo kutaka jamii
kushirtikiana kukabiliana na vitendo hivyo.
Mratibu huyo amesema uhalifu unaofanyika kwa wanyamapori na misitu ni lazima ukomeshwe kwa manufaa ya wananchi .
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero akizungumza katika mkutano huo.
Alisema
Tanzania inastahili kupongezwa kwa kuitisha mkutano wa kujadili
ujangili Mei mwaka huu na sasa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda wa
kukabiliana na ujangili.
Alisema
Umoja wa Mataifa utaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mamlaka
mbalimbali zinazoendelea kukabiliana na ujangili na kupotea kwa misitu
duniani ili kuhifadhi urithi wa dunia.
Alisema
Umoja huo kupitia mashirika yake mbalimbali watawezesha mambo
mbalimbali ili kukabiliana na ujangili na uharibifu wa misitu.
Alisema
itaendelea kusapoti programu zinazokuza uchumi wa wananchi waliopo
karibu na hifadhi za wanyamapori na misitu ili waone umuhimu wa
kushiriki kuhifadhi wanyama na misitu husika.
Balozi
wa Finland nchini Tanzania, Mh. Sinikka Antila pamoja na Balozi wa
Ujerumani nchini, Egon Kochanke nao ni miongoni mwa wadau wanaohudhuria
mkutano huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano),Ummy Mwalimu akishiriki mkutano huo.
Mwenyekiti
wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya
wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush
Arha akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Mali asili na utalii, Mh.
Lazaro Nyalandu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP)
Bw. Philippe Poinsot (katikati) akimsikiliza mdau kutoka AWF akitoa
maoni yake kwenye mkutano huo uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha.
Pichani
juu na chini ni washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda
unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu uliofunguliwa rasmi leo
jijini Arusha.
JK AOMBA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KUKABILI UJANGILI
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza kwa niaba ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye
ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya
wanyamapori uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi Wetu
RAIS
Jakaya Kikwete ameitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania
katika kukabiliana na majangili wanaomaliza tembo kwa lengo la kupata
pembe zao.
Alisema kutokana na biashara nzuri ya pembe hiuzo duniani majangili wamekuwa na soko tayari kiasi cha kuendeleza vitendo vyao.
Alisema
mitandao iliyopo inawezesha kuuawa kwa tembo hao na kufikishwa bidhaa
za pembe katika soko haramu ambalo lipo duniani na hivyo bila
ushirikiano wa kimataifa wanyama hao ambao ni urithi wa dunia watatoweka
kabisa katika miaka ijayo.
Amesema takwimu zilizopo sasa nchini za tembo zinatisha.
Alisema
mathalani kwa ujangili pekee kwenye mfumo wa ekolojia wa Selou-Mikumi
tembo waliobaki ni 13,084 kwa mwaka jana kutoka Tembo 109,419
waliokuwepo mwaka 2006.
Alisema
mfumo uliopo wa ujangili na soko la bidhaa hizo unafanya vita
inayoendeshwa na Tanzania kuwa ngumu kama haitapata ushirikiano na
mataifa mengine.
Alisema
kutokana na ukweli huo wanataka mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa
kuingia katika mapambano ya kudhibiti biashara hiyo na hivyo kuwamaliza
majangili na kuendelea kuhifadhi Tembo.
Katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili
na hifadhi endelevu ya wanyamapori, alisema serikali ya Tanzania
imeanzisha mchakato wa kulinda wanyama pori.
Baadhi ya wadau kutoka nchi mbalimbali wanaohudhiria mkutano huo
akiwemo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(wa pili kushoto).
Mchakato huo ni pamoja na kuimarisha doria , kuendesha operesheni za kukabiliana na ujangili.
Alisema
pamoja na kuwapo kwa juhudi za makusudi za kukabiliana na ujangili
serikali ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali
zikiwemo za kifedha na raslimali watu.
Aidha kumekuwepo na ushiriki mdogo kutoka kwa wananchi katika vita dhidi ya ujangili.
Alisema
kutokana na haja ya kukabili ujangili na kuwa na hifadhi endelevu,
Februari mwaka huu mataifa ya Botswana, Chad, Garbon na Ethiopia
yalitiliana saini mkataba wenye lengo la kupunguza mahitaji ya bidhaa za
wanyamapori, kuimarisha sheria zilizopo dhidi ya ujangili na pia
hifadhi na kusaidia maendeleo ya maeneo yanayokabiliwa na changamoto ya
uwindaji haramu.
Rais
Kikwete alisema katika hotuba yake kwamba kuwepo kwa mataifa hayo
katika mkutano huo ni kuendeleza makubalino ya kutojishughulisha na
biashara za bidhaa za wanyamapori kwa miaka 10 au hadi hapo tembo
waliopo bara la Afrika watakapokuwa wameondoka katika hatari ya
kuangamizwa katika uso wa dunia na majangili.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,
akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi
endelevu ya wanyamapori uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha kwenye
ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha
rais alisema kwamba mkutano huo wa Arusha unatarajiwa kuona namna ya
kuendelea utekelezaji wa makubaliano ya London, Uingereza ya hifadhi ya
wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka akiwemo Tembo.
Alisema
kutokana na mfumo wa ikolojia na hifadhi ya wanyama na majirani zake,
Tanzania inataka majirani kushiriki katika kulinda na kuhifadhi ikolojia
hiyo na wanyama waliopo na sio kuiachia Tanzania pekee.
Tanzania
ikiwa na eneo la kilomita za mraba 943,000 asilimia 30 ya eneo lake na
15 imetumika kwa hifadhi ya wanyamapori na misitu.
Amesema
eneo hilo hutumiwa zaidi kwa ajili ya utalii wa wanyamapori ambapo
asilimia 17 ya pato la taifa linatokana na utalii huo.
Wakati
huo huo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez ,ameipongeza Tanzania kwa kuitisha kikao cha kujadili ujangili
na uhifadhi endelevu wa misitu.
Mwenyekiti
wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya
wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush
Arha akiwakaribisha wadau wanaoshiriki mkutano huo kutoa maoni yao
katika udhibiti wa ujangili ulioshika kasi.
Akizungumza
kwa niaba ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Kenya na Msumbiji
alisema Umoja wa Mataifa unajisikia furaha kuona mataifa wanachama
yanakabilian na changamoto ya ujangili na uhifadhi wa misitu kwa namna
ambavyo itasaidia kizazi kijacho.
Mratibu huyo alisema kwamba ujangili unatishia maendeleo, mazingira na usalama kitu ambacho Umoja wa Mataifa unakipiga vita.
Anasema
biashara ya bidhaa za wanyamapori zinahatarisha uwepo wa wanyama ambao
tayari wapo katika hatari ya kutoweka, unasababisha rushwa na migogoro
ambayo inahatarisha maihsa ya watu.
Alisema kwa sasa dunia imekuwa ikipungukiwa na tembo wa Afrika kwa kasi
isiyokubalika kutokana na vitendo vya majangili na hivyo kutaka jamii
kushirtikiana kukabiliana na vitendo hivyo.
Mratibu huyo amesema uhalifu unaofanyika kwa wanyamapori na misitu ni lazima ukomeshwe kwa manufaa ya wananchi .
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero akizungumza katika mkutano huo.
Alisema
Tanzania inastahili kupongezwa kwa kuitisha mkutano wa kujadili
ujangili Mei mwaka huu na sasa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda wa
kukabiliana na ujangili.
Alisema
Umoja wa Mataifa utaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mamlaka
mbalimbali zinazoendelea kukabiliana na ujangili na kupotea kwa misitu
duniani ili kuhifadhi urithi wa dunia.
Alisema Umoja huo kupitia mashirika yake mbalimbali watawezesha mambo
mbalimbali ili kukabiliana na ujangili na uharibifu wa misitu.
Alisema itaendelea kusapoti programu zinazokuza uchumi wa wananchi
waliopo karibu na hifadhi za wanyamapori na misitu ili waone umuhimu wa
kushiriki kuhifadhi wanyama na misitu husika.
Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mh. Sinikka Antila pamoja na Balozi
wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke nao ni miongoni mwa wadau
wanaohudhuria mkutano huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano),Ummy Mwalimu akishiriki mkutano huo.
Mwenyekiti
wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya
wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush
Arha akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Mali asili na utalii, Mh.
Lazaro Nyalandu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP)
Bw. Philippe Poinsot (katikati) akimsikiliza mdau kutoka AWF akitoa
maoni yake kwenye mkutano huo uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha.
Pichani
juu na chini ni washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda
unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu uliofunguliwa rasmi leo
jijini Arusha.
0 comments:
Post a Comment