SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, October 24, 2014

PSPF YAFANYA SEMINA NA WALIMU WA MIKOA YOTE YA TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara iliyofanyika jana mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Katikati), akiwasili kwenye ukumbi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara, iliyofanyika mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ni muendelezo wa Mfuko, kutoa elimu kwa wanachama wake kutoka makundi mbalimbali.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akisalimiana na Hafsa Mrisho, Mkurugenzi wa Utawala na  Rasilimali watu Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa baadhi ya askari polisi na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa ya Tanzania bara wanaohudhuria semina iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro jana. Katikati ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul.
 Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiimba sambamba na baadhi ya walimu na maafisa wa Mfuko huo, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro.
 Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiimba.
 Msanii Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiimba sambamba na baadhi ya walimu na maafisa wa Mfuko huo, wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF, kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu wanaohudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya Polisi Morogoro, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mfuko huo kwa wachezaji hao na wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, wanaohudhuria semina ya siku moja iliyuoandaliwa na Mfuko huo Mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, akiwasalimia wajumbe wa semina wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa na PSPF
Mwanachama.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara iliyofanyika mkoani Morogoro. Picha na Mpiga Picha Wetu

0 comments:

Post a Comment