Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge(katikati) akiwa na
Viongozi wa Forum CC, kutoka kulia ni Oscar Munga, Mjumbe wa bodi ya
wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita, Afisa Miradi, Fazal Issa na Adam
Anthony.
===
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge (wa kwanza kushoto) akizungumza na Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita na Afisa Miradi wa ForumCC Fazal Issa.
Meneja Ushawishi wa Oxfam, Eluka Kibona wa kwanza kushoto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014.
Afisa Miradi wa ForumCC, Fazal Issa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Waandishi wa habari wakifuatilia ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa asasi za kiraia kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014.
(Picha zote na tabianchi blog).
===
Asasi
Nne zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko
ya tabianchi nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimetoa
tamko la pamoja kuhusiana na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko
ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani tarehe 23/09/2014.
Katika
tamko hilo ambalo pia limewasilishwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge, mambo matano
yamependekezwa kuzingatiwa wakati wa mkutano huo ambao Rais wa Tanzania
DK. Jakaya Kikwete pia atatoa hotuba yake.
Mambo
hayo ni pamoja na kupunguza utoaji wa hewa ukaa (Emission Reduction),
Misaada ya Fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climate
Finance), Kuongeza mapambano ya mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo,
Matumizi ya teknolojia na Nishati Mbadala na Kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge (wa kwanza kushoto) akizungumza na Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita na Afisa Miradi wa ForumCC Fazal Issa.
Meneja Ushawishi wa Oxfam, Eluka Kibona wa kwanza kushoto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014.
Afisa Miradi wa ForumCC, Fazal Issa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Waandishi wa habari wakifuatilia ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa asasi za kiraia kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014.
(Picha zote na tabianchi blog).
0 comments:
Post a Comment