Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarania Tanzania, Mohamed Mpinga na Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Afrika Mashariki, Macharia Irungu wakipiga makofi mara baada
ya kuzindua vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili
na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana.
Picha ya
pamoja mara baada ya uzinduzi wa vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya
Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini
Dar es Salaaam jana.
Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabara Tanzania,
Mohamed Mpinga akimkabidhi William Dafta
koti maalum la kuaksi mwanga mara baada ya kuzindua vilainishi vya GAPCO
RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu wakati wa hafla fupi
iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana.
Waendesha
pikipiki (maarufu kama Bodaboda) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua
vilainishi vya GAPCO RELSTARALPHA 4T vya Pikipiki za miguu miwili na mitatu
wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa jijini Dar es Salaaam jana huku wakiwa
wamevalia makoti maalumu ya kuaksi mwanga yaliyotolewa na Kampuni hiyo ili
kujilinda na usalama wao.
******
Kampuni ya Gapco
Tanzania Ltd leo hii imezindua kilainishi kipya cha
pikipiki kilijulikanacho kama Relstar Alpha 4T Ultra. Uamuzi wa Gapco kuzindua bidhaa hii ni kutokana na ongezeko kubwa
la pikipikinchinihaswakwamatumiziyakibiashara.
Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi huo,
MkurugenziMkuuwaGapco,
Bwana. MachariaIrungualisema,
“Utafiti umetuonyesha kwa sasa watumiaji wamiliki wengi wa pikipiki wanalazimishwa kutembelea gereji mara mbili kwa mwezi kwa ajili ya kurekebisha pikipiki zao.
Kupitia kilainishi chetu
cha Relstar Alpha 4T Ultra
tunawahakikishia wateja wetu kutumia muda mfupi kwenye warsha na kupata maili zaidi kwa pesa zao.
Ongezeko kubwa
la pikipiki au bodaboda nchini imeleta pia ongezeko la
vilainishi vya pikipiki vyenye viwango vya chini.Kupitia kilainishi kipya cha
Gapco wateja wataweza kupata;
maili zaidi na akiba wanapoenda kufanya marekebisho kwenye pikipiki zao.
Naye Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,
Kamanderwa Trafiki, Bwana. Mohamed
Mpinga aliwaonya watumiaji wa pikipiki kuepukana na vilainishi vya viwango vya chini na pia kuwahimiza kutii sheria za barabarani.
0 comments:
Post a Comment