Jeshi la Polisi linamshikilia Raia wa
Vietnam Dong Van(47) kwa kumkamata akiwa na meno 65 na kucha 447 za
Simba kinyume cha sheria vyenye thamani ya Shilingi Milioni 189,420,000.
Kamishna Msaidizi wa Polisi wa Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Hamisi Selemani, amesema
mtuhumiwa huyo alikamatwa jana wakati alipotaka kusafirisha nyara hizo
kwa kutumia Shirika la Ndege la Qatar Airways kwenda nchini Vietnam
kupitia Doha.
Amesema alipopekuliwa alikutwa na
nyara hizo ambazo alizihifadhi kwenye pakiti 7 za kahawa na pakiti moja
ya mchele na kuzichanganya na pakiti nyingine 15 za vyakula vya aina
mbalimbali
Kamanda Selemani amesema pakiti hizo
ziliwekwa ndani ya begi la nguo ili kupoteza ushahidi wa aina ya mzigo
alioubeba kwa wakaguzi wa uwanjani hapo.
Aidha amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Chanzo: Times Fm...
0 comments:
Post a Comment