Bw. Karl
Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa wanafunzi wa
Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013 Dorice
Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.
Miss
Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya mwezi
mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ambapo
wamepata nafasi ya kwenda kutembelea Kiwanda cha Kilimo kilichoanzishwa
mwaka 1972 ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz Knoop , mwenye uzoefu
wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania
mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina la Reila amabavyo
pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na kwa Afrika ni Tanzania pekee
tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia ya kutengeneza
umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana kukuza sekta ya
kilimo Tanzania.
Dorice
Mollel amesema “ hichi ni kitu cha muhimu sana nikiwa kama mrembo
nikirudi nyumbani na kuieleza jamii inayonizunguka ili kutuletee faida
baadae nchini kwetu”.
MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL ATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA UMEME WA GESI NA KUTUNZA MAZAO RIELA NCHINI UJERUMANI.
(Martha Magessa)
0 comments:
Post a Comment