SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, July 6, 2014

UZINDUZI WA MASHINE ZA ATM ZA SELCOM ZAFANA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza kina mama waliotembelea kutoa pesa wakati wa uzinduzi wa mashine ya ATM ya kampuni hiyo ambazo zinatoa  pesa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu kama M-pesa,tigo pesa,Airtel Money, walipo tembelea katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere. Kushoto ni Ester Kariwa na Joyce Mtema.
Mmoja ya wateja waliotembelea banda la kampuni ya Selcom Wireless, Bi,Joriet Benjamin akichukuwa fedha zake katika ATM mashine mpya za kampuni hiyo wakati wa maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza Goerge Vupembe jinsi ya mashine zinavyofanya kazi.

Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Selcom Wireless  Ally Mbaga  kushoto akifurahia jambo na mteja, Bi, Rose Mombo aliyekuja kutoa pesa katika mashine ya ATM ya kampuni hiyo

Mtaalamu wa ufundi wa mashine za ATM za Selcom, Maful Awadhakitoa maherekezo ya jinsi ya kutumia mashine hizo

Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko Juma Mgori akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashine za ATM za kampuni hiyo kwa ajili ya kutolea fedha kutumia mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel Money, na Easy pesa ATM hizo zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada ya kuziona kwa mara ya kwanza katika banda la Selcom na kushudia ATM hizo mpya na za kwanza nchini kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za mkononi

Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu mashine hizo za ATM wakati wa maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere

0 comments:

Post a Comment