Mtu
mmoja amethibitishwa kufariki Dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa
vibaya baada ya moja ya Barabara iliyokuwa kwenye matengenezo kukatika
katika mji wa Belo Horezonte karibu na eneo lenye shughuli nyingi la
Lagoa da Pampulha,nchini Brazil.
Barabara
hiyo ipo kilometa 3 kutoka Mineirao Stadium,uwanja uliotumika kwa mechi
mbali mbali za kombe la dunia na utatumika kwenye nusu fainali ya Kombe
la Dunia 2014.
Barabara hii ilikuwa ni moja ya kiungo kinachounganisha uwanja wa mpira
na uwanja wa Kimataifa wa Ndege. Barabara hiyo ni mpango wa mbasi ya
mwendo kasi ambayo ilisemekana ingekuwa tayari kutoa huduma wakati wa
mashindano ya Kombe la Dunia.
Maafisa
wa kikosi cha uokoaji nchini humo wamethibitisha kwamba Dereva wa basi
hili ndie aliefariki Dunia katika tukio hilo ambapo Barabara hiyo ambayo
ni ya Juu (Fly Over) ilianguka kwenye mji wa Belo Horizonte.
(Picha zote kwa hisani ya Pedro Duarte / AFP/Getty Images)






0 comments:
Post a Comment