SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, June 20, 2014

Waziri Hawa Ghasia azindua kongamano la wiki ya utumishi wa umma Jijini Dar

pix 3
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma,katika  ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere  jijini Dar es Salaam, kongamano hilo la siku mbili linaambatana na maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
pix 1
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Henry Mambo akiwakaribisha washiriki pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia(huyumo katika picha) wakati wa ufunguzi wa kongamano la miaka 50 ya muungano katika utumishi wa umma ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
pix 2
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Hawa Ghasia (hayumo katika picha), wakati wa ufunguzi wa kongamano la miaka 50 ya Muungano katika utumishi wa umma, katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
pix 4
Watumishi wa umma na washiriki  wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma wakimfuatilia kwa makini mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Hawa Ghasia (hayumo katika picha) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere, jijini Dar es Salaam.
pix 5
pix 6
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Hawa Ghasia (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Miaka 50 katika  Utumishi wa Umma baada ya kufungua rasmi kongamano hilo la siku mbili Juni 19 na 20 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwl. Nyerere, jijini Dar es Salaam. Lengo la kongamano ni kujadili maada mbalimbali zinazohusu utumishi wa umma. (Picha na Lorietha Laurence).
pix 7