SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 23, 2014

WANATAALUMA NA WANAZUONI WA KIISLAM WAKARIBISHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN KUJADILI HATMA YA TAIFA NA VIJANA

Washiriki wakifuatilia Majadiliamo katika Kongamano la  Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani la Mwaka 2014 ambapo "Vijana Wetu, Hazina Yetu" ndio  Kauli Mbiu ya Mwaka huu.
 Dr. Salha Mohamed akichangia mada kuhusu hali za Vijana Mayatima na Jinsi Jamii ya Kitanzania inavyoshindwa kuwaangalia na kuwaokoa na Changamoto za Dunia ya Leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Prof Mohamed Badamana akifafanua jinsi gani Malezi na Maadili Bora ya Vijana yanaweza kuwa Chachu ya Nchi zetu za Kiafrika kupiga hatua za Maendeleo ya haraka.
 Bro Ali Masoud AKA Masoud Kipanya Akitoa mada ya Umuhimu wa kufahamu Kuwasaidia vijana kuwa na Fikra Kubwa kuwawezesha Kumfahamu Mungu na Mazingira Yao Kuleta Maendeleo ya Jamii na Nchi.
 Washiriki wa Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Wakimsikiliza kwa Makini Sheikh Mussa Kundecha alipokuwa akielezea Usomaji Qur'an, Ushiriki wa Katiba ya Nchi na Hatima ya Vijana.
 Wanataaluma wa Kiislam wakifuatilia kwa makini Mjadala wa Nafasi ya Vijana na Maendeleo ya Jamii ya Kitanzania Miaka Ijayo Katika Ukumbi wa JNICC - Dar es Salaam.
 Prof Mohamed Badamana wa Chuo Kikuu Cha Nairobi, Dr. Mohamed Mohamed Said, Mwanahistoria wa Tanzania na Sheikh Khaled Mtwangi wakibadilishana Mawazo wakati wa Kongamano la Kuukaribisha Mwezi Mtukufu.
 Washiriki wakiwa na Furaha Kwa Kujaaliwa Kushiriki Kongamano la Ramadhani Ambalo zaidi ya Wanataaluma  na Wanazuoni 700 walikutana na Kujadili nafasi ya Vijana na Mustakabali wa Nchi.
Baadhi ya Wanataaluma Washiriki wa Kongamano la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati wa Mapumziko na Kubadilishana Mawazo.