
Wachimba
Mchanga, wakizidi kuutanua mto Msimbazi eneo la Jangwani kwa kuendelea
kuchimba mchanga eneo hilo kama walivyonaswa na kamera ya Sufianimafoto
hivi majuzi. Wachimbaji hao wamekuwa wakizidi kuchimba mchanga eneo hilo
baada ya mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam hivi karibuni na
kukusanya mchanga kwa wingi katika mto huo. Huu ni uharibifu wa
Mazingira unaohitaji kukemewa.



