SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 26, 2014

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA JIJINI DAR LEO

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuwaongoza watanzania katika maadhinimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kila mwaka Aprili 26, 2014 kusherehekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili 26, 1964, Watanzania wengi wamejitokeza katika maadhimisho hayo wakiwemo marais wa nchi mbalimbali za Afrika, Viongozi mbalimbali na wawakilishi wa nchi katika mataifa mbalimbali ya Afrika, Nchi za kiarabuni, Asia na Ulaya.


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wakati alipokuwa anaingi uwanja wa Uhuru leo katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..Pembeni ni Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Joyce Banda wa Malawi katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.Rais Banda kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt.Mohamed Ali Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mfalme MswatiIII katika sherehe za miaka 50 ya Muungano zilizofanyika katika viwanja vya uhuru leo.
Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni katika sherehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi katika maadhimisho ya hsrehe za miaka 50 ya Muungano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta katika hsrehe za miaka 50 ya Muungano.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Mohamed Ali Shein na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwnyesherehe za Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Mfalme Mswati wa III
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal, Mfalme wa Lesotho na rais wa Malawi Dkt Joyce Banda. na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika kwnyesherehe za Miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal,  na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakishyangilia kwa furaha wakati Makomandoo wakishuka kwa miavuli uwanjani kama inavyoonekana hapo chini. Mapicha ya kumwaga baadae kidoooogo.... 

==========

 Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride...
 Paredi la askari....likiwa ni tofauti na ilivyozoeleka...
 Moshi wa rangi...
 Ndege za kijeshi zikipita kwa speed ya ajabu...
 Askari wa Jeshi akishuka kwa Parachuti....
 Askari wa Miamvuli wakishuka kutoka umbali wa Futi 4000.....
 Watoto wa Halaiki...
Wasanii wa miziki tofauti tofauti 50, walioshirikiana kuimba wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo.