Bi. Mary Mtemahanji, mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzani Modena akiimba kwa
Bi. Zainab na Bw.Peter wakikata keki ya Muungano kwa pamoja.
Picha
ya pamoja. Kushoto ni Katibu wa Jumuiya wa Watanzania Roma na pia Katibu
wa Kamati ya Diaspora Italia Bw. Andrew Chole Mhella, katikati ni Bw.
Peter na kulia ni
Mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma Bw. Kondela Buhire.
Mheshimiwa Balozi Dkt. James Msekela akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Kutoka kushoto ni Bw. Karim Msemo, Ofisa wa Ubalozi Roma; Bw. Peter na Bw. Kondela
Buhire, mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma.
Mh. Balozi akisalimiana na Ndugu Andrew Chole Mhella, Katibu wa Jumuiya ya
Watanzania Roma na pia ni Katibu wa Kamati ya Diaspora Italy.
Wadada wa Kitanzania wakipata picha ya ukumbusho. Tokea kushoto ni Bi.Lilian
Luhende, Bi. Esther Mahella, Bi Riziki Habibu na Bi. Diana Olotu.
Picha
ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa Jumuiya za Watanzania Italia na Ofisa
wa Ubalozi. Kutoka kushoto ni Katibu wa Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki
wa Tanzania- Roma, Shemasi Romanus; Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania
Italia Bw. Abdulrahmani Ali; Mwenyekiti wa Jumuiya wa Watanzania Roma,
Bw. Erasmus Luhoyo, Ofisa wa Ubalozi, Bw. Karim Msemo na Katibu wa
Jumuiya ya Watanzania Roma, Bw. Andrew Mhella. Picha Zote zimepigwa na
Mr. Karim Msemo wa Embassy of Tanzania in Italy
Watanzania
nchini Italia, Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014, walikutana mjini Roma
kwenye ukumbi wa Ubalozi uliopo Viale Cortina d’Ampezzo 185,
kusherehekea sikukuu ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar. Mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe.
Dkt. James A. Msekela. Sherehe ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
Jumuiya za Watanzania Italia, Maofisa wa Ubalozi na familia zao, Maofisa
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Roma na familia zao pamoja na
Watanzania waishio Italia.