SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 26, 2014

MARK CHILDRESS, BALOZI MPYA WA MAREKANI NCHINI TANZANIA, ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI

Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress akikaribishwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh siku ya Alhamisi April 24, 2014 alipotembelea Ubalozi huo na kujitambulisha kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula (hayupo pichani)
Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi huyo alipotembelea Ubalozi huo siku ya Alhamisi April 24, 2014 jijini Washington, DC.
Mhe. Mark Chldress akifanya mazungumuzo na Mhe. Liberata Mulamula siku ya Alhamisi April 24, 2014 alipotembelea Ubalozi huo uliopo Washington, DC na kujitambulisha kwa Balozi.
Mhe. Liberata Mulamula akifanya mazungumuzo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Mark Childress.

Mhe. Mark Childress akipokea zawadi toka kwa Balozi Liberata Mulamula
Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Mark Childress akiwa Afisa wa Desk la Tanzania katika State Department Bw. Nathan Flook.
 Balozi Liberata Mulamula pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakifanya mazungumuzo na Balozi mpya wa Marekani Mhe. Mark Childress akiwa na Afisa wa Desk la Tanzania State Department.
 Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi