SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 22, 2014

AJALI YA KIVUKO KOREA KUSINI, WALIOPOTEZA MAISHA WAFIKIA 104 MPAKA SASA

 Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuzama kwa kivuko huko Korea Kusini inazidi kuongezeka, baada ya wazamiaji kuopoa miili zaidi. Mpaka kufikia sasa tayari miili 104 imepatikana kufuatia ajali hiyo ambayo imeacha simanzi kubwa nchini Korea Kusini
Tayari watu saba wanashikiliwa kufuatia ajali hiyo ya kivuko iliyokuwa na abiria 470 iliyokuwa ikielekea katika kisiwa cha Jeju kabla ya kuzama jumatano iliyopita. Ni watu 174 tu waliofanikiwa kuokolewa katika ajali hiyo. Kivuko hicho pia kilikuwa na waalimu na wanafunzi 339 waliokuwa katika ziara maalum