Mtangazaji wa Channel 10, Salum Mkambala, akipelekwa Theatre katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Pwani.
Msanii wa kundi la Mizengwe,
Hemed Maliyaga (wa kwanza kulia) akisaidiana na ndugu pamoja na mke wa
Mkambala (wa tatu kushoto) kumpeleka mgonjwa…
...Mkambala akiingizwa Theatre.
--
HALI ya Mtangazaji wa Channel 10, Salumu Mkambala aliyepata ajali
jana alfajiri kwa kugongana na lori akiwa safarini kuelekea Morogoro
inaendelea vizuri katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na mwandishi wetu hospitalini hapo, mdogo wa mtangazaji
huyo, Ramadhani Mkambala alisema kaka yake alikuwa akielekea Morogoro na
alipofika maeneo ya Vigwaza aligongana na lori alfajiri ya jana saa 10.
30 akiwa yeye na mtu mmoja aliyempa lifti.
Hata hivyo, chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na Ramadhani kuwa ni
kutokana na barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo mengi hali
iliyosababisha gari la kaka yake kuhama upande wake na kulivamia lori.PICHA,VIDEO NA HABARI: DEOGRATIUS MONGELA-GPL
0 comments:
Post a Comment