Stori: WAANDISHI WETU
SKENDO nzito
ya Bongo Muvi imeibuliwa na baadhi ya wabunge waliopo mjini Dodoma
kufuatia kuwalipua wasanii wake kuwa, ni ombaomba balaa, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.
Kwa
mujibu wa wabunge hao ambao walitaka majina yao yasitiriwe kwa sasa,
baadhi ya wasanii hao ambao wengi ni mastaa wamekuwa wakiwazukia na
kuwapiga mizinga jambo linalowashangaza hasa wakizingatia kuwa, wapiga
mizinga hao wana majina makubwa na huonekana wakitembelea magari ya
kifahari.
Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper.
“Hivi nyie mapaparazi, mnashindwa kabisa kukomesha hii tabia ya mastaa wa Bongo Muvi? Hawa jamaa ni ombaomba sana.
“Wamekuwa
wakitupiga mizinga sana. Tunawashangaa maana wengine wana majina
makubwa, wanatembelea magari ya kifahari lakini bado wanaomba pesa
ndogo,” alisema mbunge mmoja ambaye anatoka kwenye moja ya majimbo ya
Mkoa wa Dar es Salaam.
KINACHOWASHANGAZA WABUNGE
Kwa mujibu wa wabunge hao, linalowashangaza zaidi ni kwamba wasanii hao
ambao ni wake kwa waume, wamekuwa wakipiga mizinga ya pesa ndogo badala
ya kuomba pesa za kufanyia mambo makubwa yenye mikakati mizito.
Steve Mangere ‘Steve Nyerere’.
“Mtu
anakuja, anasema anasumbuliwa na kodi ya nyumba au anasema hajala. Hivi
kweli mastaa wakubwa kama akina…(anataja jina) ni wa kuomba vijisenti
kama vya kodi ya nyumba jamani?” alihoji mbunge mwingine kati ya watano
waliokuwa wakizungumza na gazeti hili.
Waheshimiwa
hao waliendelea kuwaanika mastaa hao kwa kudai kwamba, walichogundua ni
kuwa inapotokea wakapewa hitaji lao la fedha, huishia kukaa baa hadi
usiku wa manane na asubuhi wakiamka wako vilevile kama hawakupewa.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba.
MWAKIFWAMBA ABANWA NA RISASI
Ili
kuweka sawa madai hayo mazito na yenye aibu kubwa kwa tasnia hiyo
maarufu nchini, Risasi Jumamosi lilimtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu
Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba ambaye alikiri kuwepo kwa malalamiko
hayo ya wasanii wake kuwa ombaomba!
HUYU HAPA MWAKIFWAMBA
“Ni kweli kabisa. Mimi mwenyewe nimewahi kusikia malalamiko hayo, lakini
unajua tena ni mambo binafsi, mtu anapiga mizinga kwa mambo binafsi si
rahisi kumwingilia,” alisema rais huyo.
Aliendelea kusema kuwa, katika vikao mbalimbali vya kisanii, amewahi
kuweka wazi msimamo wa taasisi kwamba kila msanii aishi maisha yenye
heshima huku akiwa mbali na mazingira yenye kusababisha aibu katika
jamii.
KUMBE HATA JK ALIWAHI KUMLALAMIKIA
Katika kuonesha hasira zake juu ya tuhuma hizo zenye dharau katika gemu
la filamu, Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, katika
moja ya mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete
‘JK’ aliwahi kumlalamikia kwamba, wapo mastaa ambao kazi yao ni kupiga
mizinga isiyo na tija.
“Rais mwenyewe aliwahi kuniambia kuna wasanii wakiwasiliana na yeye wanamwambia mambo ya pesa za kula.
“Kuna msanii aliwahi kumtumia meseji JK akimwambia, ‘mjukuu wako leo hali mbaya’,” alisema Mwakifwamba.
Akaendelea:
“Sasa we’ unakutana na rais badala ya kumweleza mikakati mikubwa na
nini cha kusaidiwa kuifanya tasnia iweze kuendelea, unapiga mizinga
hujala, ni aibu sana.”
WALISHAMPIGA ‘MIZINGA’ HADI ‘MTOTO WA MKULIMA’
Mwakifwamba hakukubali kufumba midomo yake bila kupasua yote ambapo
alizidi kudai kuwa, hawashangai sana wasanii wake hao kwani waliwahi
kumpiga mizinga hadi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ‘Mtoto wa Mkulima’.
“Niliwahi kukutana na Waziri Mkuu Pinda, nikamwomba mambo ya kuisaidia
tasnia ya filamu Tanzania, akasema afadhali mimi nimeongea vitu vya
maana, kuna wenzangu alikutana nao ‘wakambomu’ fedha za matumizi
binafsi, nilishangaa sana,” alisema Mwakifwamba.
RISASI LAWASAKA MASTAA, WAPATIKANA HAWA:
Jacqueline Wolper, ni staa wa filamu za Kibongo. Filamu yake ya kwanza
ni Ama Zao Ama Zangu. Yeye alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema:
“Ni kweli, sikatai kwamba hiyo tabia ipo tena sana tu. Lakini
wanaoongoza ni mastaa wa kiume, hao ndiyo wanaotutia aibu ya kuonekana
sisi ni o
mbaomba.”
STEVE NYERERE
Yeye ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity. Alisema anavyojua kuna kuonana kirafiki na waheshimiwa na kuonana kiajenda.
“Tabia ya kuomba fedha kwa waheshimiwa ipo. Lakini linapokuja suala la
tasnia yetu kupeleka hoja kwao, tunaanza hoja baada ya hapo kuna
waheshimiwa wengi wana urafiki na wasanii, tunaitana pembeni na kupiga
kirungu.
“Siwezi kukaa na waheshimiwa kama Rostam Aziz, William Ngeleja,
Mheshimiwa Abood na Nimrod Mkono halafu nikawaacha hivihivi, kisa eti
mimi ni Mwenyekiti wa Bongo Muvi,” alisema Steve akionesha kumshangaa
mwandishi aliyempigia simu kutaka usawa wa mizani ya habari hiyo.
Jennifer Kyaka ‘Odama’.
ODAMA YEYE
Jennifer
Kyaka ‘Odama’ yeye alipata umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Odama
iliyokuwa ikirushwa na Televisheni ya Taifa (wakati huo TVT).
Alipopigiwa simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa licha ya kurudiwa
mara kadhaa.
Aunt Ezekiel
AUNT EZEKIEL
Risasi
pia lilimtafuta nyota mwingine aliye mahiri kwenye sinema za Bongo,
Aunt Ezekiel ambaye filamu iliyompaisha sana inaitwa Miss Tanzania. Yeye
simu yake ya mkononi ilionesha kutokuwa hata na laini kwa wakati huo.
Staa mkongwe katika gemu, Vincent Kigosi ‘Ray’.

RAY AFUNGUKA
Staa
mkongwe katika gemu tangu enzi za Kaole Sanaa Group, Vincent Kigosi
‘Ray’ aliposakwa na kuulizwa kuhusu madai hayo ya wasanii kuwa ombaomba
alisema:
“Wasanii
wengi wanawaza maisha ya hapa na si baadaye. Badala ya mtu kuweka shida
zake kwenye mfuko wa karatasi, anaweka kwenye rambo ambao unapiga
kelele.
“Mwisho
wa siku anaomba shilingi milioni tatu akagombolee gari au asaidiwe kodi
ya nyumba, anasahau kuwa kapata nafasi ya kuonana na mheshimiwa
azungumzie tasnia tunavyonyonywa hadi kuuza hati miliki,” alisema Ray.CREDIT GPL









0 comments:
Post a Comment