Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mhe. Nabil Fahmy wakizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya siku
tatu ya Mhe. Fahmy hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari,
2014. Mhe. Fahmy yupo nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya
nchi hizi mbili hususan katika nyanja za afya, elimu, uwekezaji na
siasa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Nabil Fahmy (hayupo pichani) katika
mazungumzo rasmi yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency
(Kilimanjaro) Jijini Dar es Salaam. Mhe. Fahmy yupo nchini kwa ziara ya
kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari, 2014. Wakati wa
mazungumzo hayo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na
kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususan katika nyanja za
elimu, afya na uwekezaji. Kulia kwa Mhe. Membe ni Mkurugenzi wa Idara ya
Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Vincent Kibwana.
Mhe. Fahmy akieleza jambo wakati wa mazungumzo.
Mhe. Fahmy nae akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana (kushoto waliokaa) na Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga wakinukuu mazungumzo kati
ya Mhe. Membe na Mhe. Fahmy (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao na
Waandishi wa Habari.
Mhe. Fahmy (wa nne kutoka kushoto) kwa pamoja na ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mkutano wao.
Ujumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Fahmy (hawapo pichani)
Mhe. Membe akizungumza.
Mhe. Membe na ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Fahmy (hayupo pichani)
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe
na Mhe. Fahmy (hawapo pichani).
0 comments:
Post a Comment