
Mjumbe wa Bunge Maalumu la katiba Mhe Maria Sarungi akiwa na wawakilishi wa wasanii hao mjini Dodoma

Kikao kimoja kati ya vingi vya wasanii na wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba

Kikao kikiendelea..

Hapa lazima kieleweke

Tunadai haki yetu ya wasanii

Mhe William Ngeleja na wawakilishi wa wasanii wa muziki na uchoraji

Mhe Joseph Mbilinyi a.k.a Mr Sugu akihutubia wawakilishi wa wasanii

Wasanii lazima tuwakilishwe...

Mhe Sugu na wasanii

Mikakati ya wasanii ikiongelewa

Viongozi wa kundi la wasanii

Mhe Martha Mlata anaungana na wasanii wenzie

Tuko pamoja

Mhe Samwel Sitta na wasanii

Mhe Iddi Azzan akiwajibika kwa wasanii

"...Sikiliza Mheshimiwa Sitta...Wasanii ni kundi muhimu sana katika jamii... Hivyo mkitusahau mtajiju....
Wasanii
12 wakiwemo viongozi toka Shirikisho la muziki, Shirikisho la Filamu,
Shirikisho la Sanaa za ufundi, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania walifunga
safari na kuvamia Dododma na kuwa na mfululizo wa mikutano na wabunge
mbalimbali ili kuwashawishi waunge mkono vipengele viwili ambavyo
wasanii wanavitaka katika Katiba
1. Kundi la wasanii kutambuliwa katika Katiba kama vile walivyotambuliwa Wakulima, wafugaji, wavuvi na wafugaji walivyotajwa
2.
Milliki Bunifu kwa kiingereza Intellectual Property ambamo ndani yake
kuna Hakimiliki itajwe rasmi katika Katiba hili litawezesha sheria
mwafaka zitungwe katika kuendeleza sanaa na kulinda kazi za sanaa na
kazi za ubunifu. Kundi hili limepokelewa vizuri sana na wabunge wote
lililokutana nao
0 comments:
Post a Comment