Mama
wa Mitindo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa
onesho la Lady in Red, Bi. Asia Idarous Khamsin akizungumza na wadau
tasnia ya mitindo waliojumuika kwenye After Party ya kuwashukuru wadau
waliotoa michango mbalimbali tangu kuanza kwa onyesho la Lady in Red
nchini Tanzania.
Mama
wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin akipozi wakati wa zoezi la kugawa
vyeti na models waliovaa mavazi yaliyoonyeshwa kwenye onyesho la
kutimiza miaka 10 la Lady in Red lililofanyika hivi karibuni.
Mwanamitindo
wa siku nyingi Fiderine Iranga akipokea cheti kutoka kwa Mama wa
mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kutambua mchango wake katika tasnia ya
mitindo nchini.
Mwanamitindo
mkongwe Fiderine Iranga akimkabidhi zawadi Mama wa Mitindo Bi. Asia
Idarous kwenye After party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe
za kutimiza miaka 10 ya onyesho la Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa
juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar.
Mbunifu
wa mavazi nchini Ally Rehmtullah akipokea cheti cha shukrani ya
ushiriki wa onesho la Lady in Red kutoka kwa mama yake mlezi Asia
Idarous Khamsin.
Cake
ya After Party ya Onesho la Lady in Red iliyoandaliwa maalum kwa
kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha sherehe za miaka 10 ya Lady
in Red nchini.
Honest
Arroy wa 360 Degrees akikata cake kwa niaba ya wadau kwenye After Party
ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani
Lounge.
Model
Richard akilishwa kipande cha cake na Mama wa Mitindo Asia Idarous
Khamsin kama shukrani ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya Lady in Red.
Wadau
mbalimbali waliojitokeza kwenye After Party ya kusherehekea miaka 10 ya
Lady in Red wakitazama matukio mbalimbali kwenye luninga ndani ya kiota
cha Nyumbani Lounge.
Mwandishi
wa gazeti la Tanzania Daima, Andrew Chale akilishwa kipande cha cake na
mmoja wa Models kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha
tangu kuanzishwa onesho la Lady in Red mpaka leo hii kutimiza miaka 10
kwenye tasnia ya mitindo nchini.
Wadau
wakiwa wamepozi kwenye kiota cha Nyumbani Lounge wakati wa After Party
ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mdau akipata Ukodak na Models.
Mama
wa Mitindo nchini Asia Idarous Khamsin akipata ukodak na mwanamitindo
Mustafa Hassanali kwenye After Party ya kuwashukuru wadau walioshiriki
kwenye onesho la Lady in Red lililotimiza miaka 10 hivi karibuni.
Na Andrew Chale
HAFLA maalumu
ya kilele cha Miaka 10 ya onesho la mavazi la ‘Lady in Red Super Brand’
usiku wa Jumamosi Februari 22, lilikuwa la aina yake kwa kuvutia watu
mbalimbali ndani ya ukumbi na mgahawa wa kisasa wa Nyumbani Lounge,
ambapo pia wadau walikabidhiwa vyeti.
Tukio hilo la
aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa wakiwemo wadau wa ubunifu na
mitindo nchini pamoja na watu maarufu, pia walipata kupita kwenye zulia
jekundu (red carpet) na kupata picha za ukumbusho wa tukio hilo.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho hilo kila
mwaka, Asia Idarous Khamsin, aliwashukuru wadau waliojitokeza kwenye
hafla hiyo maalumu na kutoa vyeti kwa watu na taasisi zilizoweza
kuliunga mkono onyesho hilo pamoja.
Wengine ambao nao wanachipukia kwa sasa akiwemo Salim Ally, Salim Ally, Abdul Mwene,Baby Julieth, Baby Masai na wengine wengi.
Asia Idarous
alibainisha kuwa, wapo mbioni kuliboresha jukwaa hilo na kuwa la
kimataifa ikiwemo kushirikisha wabunifu wa kimataifa na kufungua milango
kwa wabunifu wa ndani kujiuza kimataifa.
Aidha, katika
halfla hiyo pia wageni na wadau waliofika walipata kushuhudia shoo fupi
ya mavazi yaliyobuniwa na Lucy Warere wa Tifu Tifu Fashions, Beda Masai
na Asia Idarous Khamsini.
Asia Idarous
aliwataja wadhamini waliodhamini halfa hiyo ni pamoja na Times FM,
Michuzi Media group, MOblog, DTV, Nyumbani Lounge, Darling Air, G one
Media, Channel Ten, CTN na wengine wengi.
“Tunamshukuru
Mungu kwa kufikisha Miaka 10 ya Lady in Red, hadi kufikia hapa,
tumeweza kufanya mambo makubwa katika tasnia hii ya ubunifu wa mavazi na
jukwaa hili litaendelea kuwa chachu ya mafanikio zaidi na zaidi,”
alisema Asia Idarous.
Aliongeza
kuwa, jukwaa hilo ndilo pekee lililoweza kuibua wabunifu wakubwa hapa
nchini huku wengine wakipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi,
wabunifu hao ni pamoja na Ally Rehmtullah, Martin Kadinda, Ahmed Abdul,
Faustin Simon.

















0 comments:
Post a Comment