Wadau mbali mbali wa mchezi wa Soka jijini Dar es Salaam,leo wamekutana
pamoja kwenye viwanja vya Tabata Shule katika Bonanza la kumuenzi
Marehemu Omary Changa (pichani) aliyewahi kuwa Mchezaji katika timu za
Yanga,JKT Ruvu,Kagera Suger pamoja na Moro United aliefariki dunia mwezi
uliopita.Bonanza hilo limefanyika maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha
za kuisaidia familia ya Marehemu Changa ikiwa ni pamoja na kuweza
kufanikisha kisomo cha Arobaini yake.
Mshambuliaji wa Pembeni wa timu ya Kijitonyama Veterans,Majuto Omary
akichanja mbuga katika lango la wapinzani wao ambao ni Tabata
Veterans,wakati wa Bonanza la kumuenzi Marehemu Omary Changa (pichani)
aliyewahi kuwa Mchezaji katika timu za Yanga,JKT Ruvu,Kagera Suger
pamoja na Moro United aliefariki dunia mwezi uliopita,lililofanyika leo
kwenye Uwanja wa Tabata Shule,jijini Dar es Salaam.
hapiti mtu hapa.......
Beki wa Kati wa timu ya Kijitonyama Veterans akiondoka na mpira huku mpinzani wake akimsindikiza.
Hapa ni vumbi tuuuuu........
Kiungo mchezeshaji wa timu ya Kijitonyama Veterans,Ally Ferooz
akionyenya umahiri wake mbele ya mabeki wa timu ya Tabata Veterans.
imekubaliiii....
anakwenda na mpiraaaa......
hapa ni Unyenyembe FC na Tabata Rangers
Beki wa Unyenyembe (Mwenye Blue) akichuana na wachezaji wa timu ya Tabata Rangers.
Straika wa timu ya Unyenyembe FC,Othman Tippo a.k.a Zizzou (kushoto)
akiwacheki wachezaji wa Tabata Rangers wakati akipiga mpira wa adhabu.
Beki kazi yake ni Kuzuia.
Maalim Tippo akionyesha uwezo wake.
KWA HISANI YA ISSA MICHUZI
0 comments:
Post a Comment