Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels
Moment, Bi Naima Malima akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda
akitoa ushuhuda wake juu ya kutumia fursa katika ujasiriamali. Mama Tunu alishiriki
katika Tamasha hilo akiwa mjasiriamali aliyekuwa akiuza mazao yatokanayo na
nyuki.
Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu
wa Rais, Mama Asha Bilali akisoma hotuba yake wakati akifungua Tamasha hilo la
kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda
akimuonesha bidhaa zilizomo bandani kwake alipotembelewa na Mgeni Rasmi wa
Tamasha hilo, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.
Kulikuwa na utaoji wa tuzo kwa
washiriki katika Tamasha hilo. Bila kusahau burudani kutoka THT, ambao
waliigiza mahudhui ya Tamasha.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels
Moment, Bi Naima Malima akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa
Makamu wa Rais, Mama Asha Bilali.
Baadhi ya kina mama waliojitokeza
kuhudhuria Tamasha hilo.
Wake wa Viongozi (New Millenium Women
Group) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo, Mke wa Makamu
wa Rais, Mama Asha Bilali.Picha zote na Saidi Ahmed Mkabakuli
0 comments:
Post a Comment