SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, January 8, 2014

WANAFUNZI BORA WA SAYANSI WAENDA DUBLIN IRELAND

 Mwakilishi  kutoka  Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo  ya Singida, Jafari Ndagula mmoja wa washindi wawili wa jumla wa  shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo pichani) wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za  Tuzo  za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST  zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.
 Mwakilishi  kutoka  Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Fidel Castro ya Zanzibar, Muslih Othman Khamis, mmoja wa washindi wa shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyonyika jijini Dar es Salaam jana. Tuzo hizo zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.

0 comments:

Post a Comment