SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, January 25, 2014

Taasisi ya Catherine Magige kulisha watoto wa Levolosi mwezi mzima

Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (kushoto) akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili ya uji wa wanafunzi shule ya msingi Levolosi. Wanao pokea ni Mwenyekiti Kamati ya Shule, Edward Ngomuo (kulia) Mwalimu Mkuu Shule ya Luvolosi, Elisante Kaaya na Mwalimu wa Chakula shuleni hapo, Frida Mallya.

*********
JAMII imetakiwa kuwa na moyo wa kujitolea na kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii hasa wanawake na watoto ili kujenga taifda lenye matumaini na amani.

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation, ya jijini Arusha, Catherine Magige wakati akikabidhi msaada wa unga wa sembe na sukari kwaajili ya kuwapikia uji wanafunzi zaidi ya elfu moja katika shule ya Msingi Levolosi ya mjini hapa kwa muda wa mwezi mmoja.

Magige ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM) mkoa wa Arusha, amesema kila mtu anapswa kujipima kwenye mizani ya ubinadamu, kujitafakari na pia kujiuliza maswali magumu kwenye nafsi yake, kwamba, katika kipindi kifupi cha uhai wake, ameacha nyuma matunda ya aina gani.

“Tunapaswa tusambaze mbegu za matunda ya amani na upendo na si mbegu za machafuko…kwani ndio mbegu ambazo sote tunapaswa kuzisambaza na kuzipanda ili kujenga taifa lenye matumaini na amani,”alisema Magige.

Ni ukweli usio pingika kuwa watoto wetu hawa tusipo wawezesha kupata elimu sasa basi tutakuwa tumejingeneneazea wenyewe taifa la watu mbumbumbu na wasio na ujuzi wa kufanya jambo lolote jema na matokeo yake wataishia katika magenge ya uhalifu na watumiaji wa madawa ya kulevya.

Magige amesema ili watoto wafanye vizuri darasani wanahitaji kushiba na si familia zote zinamudu kuwapa chakula watoto wao kabla ya kwenda shule hivyo taasisi yake ya Catherine Foundation imeona ichangie kulisha watoto hao kwa mwezi mmoja.

“Sisi kama wazazi hatuna budi kusaidia wazazi wengine ambao wanania njema na watoto walio wazaa isipokuwa uwezo ndio unawakwamisha katika kutimiza malengo yao ya kuwasaidia watoto wao katika elimu,” alisema Magige.

Aidha amesema utaratibu wa kuwapa watoto chakula shule utaongeza kiwango cha usikivu wa wanafunzi darasani na kuongeza ufaulu huku ukupunguza tatizo la utoro mashuleni ambalo limekithiri katika shule nyingi nchini.

“Kufanya hivi situ watoto watakuwa wasikivu darasani bali hata kuchangia kwa kiwango cha ufaulu darasani na ni wazi kuwa hata mahudhurio yataongezeka shuleni hapa,” alisema Magige.

Pia amewataka wanafunzi wanafunzi kukazania masomo yao darasani, kudumisha nidhami mingoni mwao huku akiwataka walimu kutimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwapa elimu bora na malezi stahiki watoto hao na maadili mema.

Mapema katika hotuma yake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Levolosi, Elisante Kaaya alisema shule hiyo ina wanafunzi 1,029 na gharama za kuwalisha kwa mwaka zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh Milioni 10.

Aidha Mwalimu Kaaya alisema kuwa ili kufanya zoezi hilo la kuwapa uji au chakula wanafunzu linaendelea wameazimia kuwashirikisha wazazi na wadau wengine wa elimu ili uwe endelevu na wenye kuleta tija.
Ofisa wa Catherine Foundation Lucy Bongole akizungumza jambo kabla ya makabidhiano kuanza.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Levolosi, Elisante Kaaya akitoa maelezo ya shule hiyo na mpango wa kuwapa uju wanafunzi wanafunzi 1,029 na gharama za kuwalisha kwa mwaka zinakadiriwa kuwa zaidi ya Sh Milioni 10.
Juice zikigawiwa kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Shule ya Msdingi Levolosi ya jijini Arusha, Edward Ngomuo akisema neno.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akigawa juice kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation na Mbunge wa viti Maalum Arusha, Catherine Magige akizungumza.
Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (wapili kushoto) akimuweka katika kiti maalum cha magurudumu, motto mlemavu Hassan Ramadhani (10) mkazi wa Luvolosi mjini Arusha jana. Wanaoshuhudia ni mama mzazi wa motto huyo, Hadija Hassan na Mwalimu Mkuu Elisante Kaaya wa Shule ya Msingi Luvolosi.
Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (kushoto) akikabidhi masaada wa unga wa sembe kwaajili ya uji wa wanafunzi shule ya msingi Luvolosi ya mjini Arusha jana. Anaeshuhudia ni Mwalimu Mkuu Elisante Kaaya.
Wazazi na walimu wakipokea unga na sukari
wanafunzi nao wakipokea
Wawakilishi wa wazazi wakipokea msaada huo.
Mwalimu wa Chakula shuleni hapo, Frida Mallya akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Catherine Foundation.
Mwenyekiti wa Catherine Foundation, Catherine Magige akiagana na wanafunzi.

0 comments:

Post a Comment