SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, January 3, 2014

Taarifa ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Kuhusu Kikao cha Kamati Kuu Leo

 John Mnyika-Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mbunge wa Jimbo la Ubungo-Chadema
--
   CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho,Chama kimetoa kauli ifuatayo;

Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama Leo tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano huo ni tatu;

Mosi: Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya
kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.

Pili: Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.

Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.

Tatu: Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014

Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na taifa.

John Mnyika
Mkurugenzi wa Mawasiliano

0 comments:

Post a Comment