Rais Jakaya Kikwete
----
Rais Jakaya Kikwete amesema Operesheni Tokomeza Ujangili
iliyositishwa kwa muda kutokana na utekelezaji wake kukumbwa na kasoro
na kusababisha mawaziri wake wanne kuwajibika kisiasa, itaendelea baada
ya kukamilika kwa matayarisho ya awamu yake ya pili.
Akizungumza katika salamu zake za Mwaka Mpya jana,
Rais Kikwete alisema:
“Tunakamilisha matayarisho ya kuanza awamu ya
pili ya Operesheni Tokomeza. Ni muhimu kuendelea nayo kwani tusipofanya
hivyo majangili wataendelea na vitendo vyao viovu.
“Wakati nikilihutubia Bunge Novemba 7, mwaka jana
niliagiza ifanyike sensa katika Pori la Hifadhi la Selous. Hali ni
mbaya, sensa imekamilika lakini taarifa yake inatisha. Kuna tembo 13,084
tu wakati mwaka 1976 walikuwa na tembo 109,419.”
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku
12 tangu Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilipotoa
ripoti yake iliyoeleza athari mbalimbali za operesheni hiyo, ikiwa ni
pamoja na unyanyasaji, uharibifu wa mali na mauaji ya binadamu na
mifugo.
Ripoti hiyo ilisababisha, Rais kutengua uwaziri wa
Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi), Dk
David Mathayo (Mifugo na Uvuvi) na Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na
Utalii), baada ya wizara zao kutajwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa
operesheni hiyo.
Hata hivyo, Rais alisema mtindo wa mzigo wa makosa
ya watumishi wa umma kubebwa na viongozi wa kisiasa pekee, tena
wasiokuwa na hatia ya moja kwa moja, siyo sahihi. “Lazima kila mtu abebe
mzigo wake inavyostahili. Ni matumaini yangu pia kwamba katika siku za
usoni kunapotokea matatizo ya namna hii uchunguzi uwe wa kina ili wale
hasa waliohusika na kutenda makosa wawajibishwe.
Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea......
0 comments:
Post a Comment