SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, January 7, 2014

MAMA ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE KWA MKUPUO JIJINI MBEYA APOKEA SEHEMU YA MISAADA TOKA KWA WASAMARIA WEMA

  Binti Aida Nakawala (miaka 25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya,akiwa na watoto wake wanne aliojifungua hivi karibuni katika hospitali ya Wazazi ya Meta,Jijini Mbeya.Mama huyo alijifungua Watoto hao wa wanne kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya na anaendelea vizuri kabisa.Mama huyo jana alitembelewa na baadhi ya Wadau wa Habari wakiongozwa na Mwanalineneke wa Blog ya Mbeya Yetu,Joseph Mwaisango,ambapo waliwasilisha mchango wao mdogo waliokuwa nao,wengine alioambatana nao katika kuwasilisha msaada huo ambao ni pesa taslim,simu ya mkononi na nguo za watoto hao toka kwa wasamaria wema ambao ni Yassin Kapuya , Hassan Othman,Mwanalibeneke Othman Michuzi pamoja na Dada Pendo Fundisha.
Mwanalibeneke Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog (kulia) na Dada Pendo Fundisha wa New Habari (kushoto) wakiwasilisha msaada wa nguo kwa Mama aliejifungua watoto wanne kwa pamoja,Bi. Aida Nakawala.
Mdau Ezekiel Kamanga pamoja na Mwanalibeneke Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu Blog wakikabidhi msaada wa pesa taslim pamoja na simu ya mkononi kwa kwa Aida Nakawala,mama aliejifungua watoto wanne kwa pamoja.Utaratibu wa kumpatia mama huyo namba ya simu unafanyika hivi sasa na iwapo itakuwa tayari italetwa hapa hapa ili kwa yeyote atakaetaka kumsaidia mama huyo,aweze kufanya hivyo.
Wakipata maelezo ya Maendeleo ya Mama huyo kutoka wa Muuguzi,Terecia Bahari (kushoto).
Baadhi ya wadau waliomtembelea mama huyo hospitali ya Wazazi ya Meta,jijini Mbeya.

0 comments:

Post a Comment