SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, January 19, 2014

Kampuni ya Vodacom Mjini Mbeya imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima wa zaidi ya Shilingi Milioni tatu.

Meneja wa Kampuni ya vodaco  Mbeya mjini Emmanuel Sagenge akimkabidhi mratibu wa msaada huo Zahara Mansoor
Bidhaa mbalimbali zilizokabidhiwa kituoni hapo>Meneja wa Kampuni hiyo Mbeya mjini Emmanuel Sagenge amesema kama kampuni imeguswa sana na uwepo wa watoto yatima katika jamii inayowazunguka.
 Mratibu wa zoezi hilo. Zahara Mansoor ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtandao wa watoto mkoa wa Mbeya amesema msaada huo utagawanywa katika vituo vitatu ambavyo ni Nuru, Iwambi na Chipro vyote vya jijini Mbeya.
Meneja wakituo cha Nuru Amanda Fihavango



KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Mbeya mjini imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima wa zaidi ya Shilingi Milioni tatu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo katika hafla iliyofanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Orphans Centre kilichopo Uyole Jijini Mbeya, Meneja wa Kampuni hiyo Mbeya mjini Emmanuel Sagenge amesema kama kampuni imeguswa sana na uwepo wa watoto yatima katika jamii inayowazunguka.
 Amesema kuwa ni vema makampuni mengine pamoja na taasisi mbali mbali kujenga utamaduni wa kujitolea kwa ajili ya watotro yatima na sio kluwaachia jukumu hilo wenye vituo pekee kwa sababu kazi hiyo ni ya jamii nzima ya watanzania.

Amevitaja vitu walivyotoa ambavyo vinagharimu kiasi cha fedha taslimu shilingi million tatu kuwa ni pamoja na unga wa sembe gunia 6 zenye ujazo wa kilo sita kila kimoja, sabuni katoni 6, sabuni za unga  ndoo 6, sabuni za vipande miche 6,mafuta ya kula ndoo 6, mchele kilo 60 na maharage kilo 60.

Vingine ni Peni, kalamu, madaftari, miswaki, juisi, rula, dawa za miswaki, maziwa na chumvi ambavyo vitagawanywa katika vituo vyote vitatu kulingana na mahitaji ya vituo vyenyewe.

Kwa upande wake mratibu wa zoezi hilo. Zahara Mansoor ambaye pia ni Mwenyekiti wa mtandao wa watoto mkoa wa Mbeya amesema msaada huo utagawanywa katika vituo vitatu ambavyo ni Nuru, Iwambi na Chipro vyote vya jijini Mbeya.

Amesema huo ni utaratibu wake aliojiwekea wa kutoa zawadi kwa watoto yatima kila mwaka kupitia makampuni mbali mbali yanayoguswa na uwepo wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Na Mbeya yetu

0 comments:

Post a Comment