Winga
Machachali wa Timu ya Clouds Media,Said Tully akituliza mpira kwa
umaridadi kabisa mbele ya Beki wa Timu ya Gebi Presha ya Magomeni wakati
wa Mtanange wao wa kufunga mwaka,uliofanyika kwenye Uwanja wa
Tanganyika Packers,Kawe jijini Dar.Clouds Media walilala kwa mabao 2-1
Mshambuliaji wa Timu ya Gebi Presha ya Magomeni,akiondoka na mpira.
Ilikuwa ni patashika la nguvu uwanjani hapo.
Dukiiiiiiiiii........
Hatariii langoni mwa timu ya Clouds Media.
Kiungo mshambuliaji wa timu ya Clouds Media, Shaffih Dauda akiipangua ngome ya Gebi Presha.
haya twendeeeee......
Kocha
wa timu ya Clouds Media, Alex Lwambano akiwa ameshika kiuno baada ya
timu yake kupigwa bao 2,huku akiwa na mashaka tele juu ya kibarua chake
katika timu yake hiyo.maana hii ilikuwa ni mechi ya pili kupigwa,tena
nyumbani.
Kocha Lwambano akiongea kwa unyonge na wachezaji wake ili wajitahidi kukaza.
Kocha Lwambano akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu yake wakati wa mchezo huo.
Kwa
Upande wa Gebi Presha kulikuwa na makocha wa kutosha tu,kwani kila mmoja
alitoa mawaidha kwa mchezaji wake.labda ndio maana wakaibuka kidedea.
Makocha wakimwaga cheche kwa wachezaji wao.
Umesikia wewe........
Straika Antonio Nugaz akiondoka na kijiji.
Mashabiki lukuki.
0 comments:
Post a Comment