Ismail Aden Rage ndiye Mwenyekiti
halali wa Simba ambapo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imemtaka
kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa taratibu za klabu ya Simba. (HM)
Kamati imebaini upungufu kadhaa wa
kisheria kwenye uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya Simba uliofanywa Novemba
18, 2013 kwa kumsimamisha Mwenyekiti wao. Upungufu huo ni pamoja na
ukiukwaji wa Ibara ya 33 ya Katiba ya Simba juu uitishaji wa mkutano,
ajenda ya kumsimamisha Mwenyekiti kuwasilishwa kwenye kikao kwa
utaratibu wa mengineyo.
Changamoto nyingi zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti huyo zingeweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia Ibara ya 16(2) ya Katiba ya Simba.
Hivyo, agizo za Rais wa TFF, Jamal
Malinzi kumtaka Mwenyekiti wa Simba aitishe mkutano lipo palepale. Pia
Mwenyekiti ametakiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu
Mwenyekiti kwa kuzingatia Katiba ya klabu hiyo.
Katika mkutano huo wa kujaza nafasi,
ndiyo utakaojadili mgogoro kati ya Mwenyekiti na Kamati yake ya
Utendaji. Nafasi hiyo kwa sasa inakaimiwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya klabu hiyo, Joseph Itang'are baada ya Geofrey Nyange
aliyekuwa akiishikilia kujiuzulu.
TFF inakumbusha wanachama wake wote
(vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu) kuzingatia Katiba
zao. Kamati pia imegundua ukikwaji wa maadili katika suala hili, hivyo,
litapelekwa katika kamati husika.
Kwa vile maslahi ya TFF ni kuona mpira wa miguu unachezwa kwa utulivu, itazikutanisha pande husika wakati wowote kuanzia sasa.
Kuhusu mchezaji Emmanuel Okwi ambaye
aliuzwa nchini Tunisia, TFF inafahamu kuwa klabu ya Simba bado
haijalipwa na itasaidia kufuatilia FIFA fedha za mauzo ya mchezaji huyo.
Chanzo: shaffihdauda
0 comments:
Post a Comment