Baadhi ya vipodozi vilivyokamatwa
Mifuniko ya tenki la mafuta ikiwa imefunguliwa baada ya kutolewa vipodozi
Ndani ya lori hilo baada ya kutolewa vipodozi hivyo
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa
Ramadhan Mungi akionyesha shehena ya vipodozi ambavyo vimekamatwa
vikisafirishwa ndani ya lori la mafuta leo
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ,Ramadhan Mungi akionyesha lori la mafuta lililokuwa na shehena ya vipodozi
Jina la kampuni linalomiliki lori hilo
Maofisa wa mamlaka ya chakula na dawa Manispaa ya Iringa wakikagua vipodozi hivyo
Na Francis Godwin Blog
JESHI
la polisi mkoa wa Iringa limewakamata watu wawili akiwemo
dereva wa tenki la mafuta lenye namba za usajili T 247 BHP
wakisafirisha shehena ya vipodozi maboksi 779 vikiwa vimewekwa ndani
ya tenki hilo la mafuta kutoka nchi za kusini mwa Tanzania
kuelekea jijini Dar es Salaam .(P.T)
Kamanda wa polisi wa mkoa wa
Iringa Ramadhan Mungi alisema kuwa lori hilo lenye namba za usajili
T 247 BHP likiwa na tela lenye namba T 598 BMK ni mali ya kampuni
ya World OIL Ltd ya Jijini Dar es Salaam lilikuwa likiendeshwa na
Mohamed Sadru (23) mkazi wa Mbezi Temboni jijini Dar es Salaam .
Mbali ya dereva huyo pia jeshi
hilo linamshikilia mfanyabiashara aliyekuwa akisafilisha mzigo huo
Bw Kassim Kaifa (23) mkazi wa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za
kuhusika na mzigo huo.
Kamanda Mungi aliwaeleza wanahabari
leo kuwa mtego wa jeshi la polisi uliweka baada ya kupokea
taarifa kutoka kwa rai wema kuhusiana na lori hilo kutumika isivyo
kwa kusafirisha vipodozi hivyo.
Alisema kuwa taarifa kuhusiana na
lori hilo kusafirisha vipodozi badala ya mafuta waliitapata kutoka
jana na mtego wa kulikamata lori hilo umefanikiwa majira ya saa 9
alfajiri ya leo
Hata hivyo alisema kuwa sehemu
kubwa ya vipodozi hizo ni vile ambavyo vilipigwa marufuku na
serikali kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa afya ya watumiaji
wa vipodozi hivyo.
Alisema kuwa jeshi la polisi
limefanikiwa kumata vipodozi hivyo kwa kushirikiana na mamlaka ya
chakula na dawa ,wakala wa barabara mkoa wa Iringa na mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA)
Kamanda huyo alisema kuwa watuhumiwa
hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika na
kuwa ni mapema kwa sasa kuitaja thamani ya vipodozi hivyo na
nchi ambayo lori hilo lilikuwa likitoka kutokana na sababu za
kiusalama.
MWISHO
|
0 comments:
Post a Comment