SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, December 31, 2013

Januari hadi Machi mvua kuwa za wastani kusini mwa nchi- TMA

Dr-Agnes-Kijazi
Mkurugenzi  Mkuu  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr. Agnes Kijazi.

Na Kiza Sungura-MAELEZO-

MAMLAKA ya Hali Hewa Tanzania (TMA) imesema kuwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa Januari hadi Machi 2014 mvua zinatarajiwa kuwa za wastani kwa upande wa kusini mwa Nchi na juu wastani katika maeneo ya kati na magharibi mwa Nchi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi  Mkuu  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr. Agnes Kijazi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya tathmini na mwelekeo wa mvua  nchini kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2014.

Dr. Kijazi aliongeza kuwa mvua za vuli zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka yanatarajiwa  kupata mwendelezo wa mvua za nje ya msimu katika mwezi Januari na Februari 2014.

Amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha zitakuwa katika maeneo ya kanda ya Magharibi na  kanda ya Kati zitaanzia wastani hadi chini ya wastani.

Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa kwa upande wa Nyanda za juu Kusini Magharibi na Kanda ya Kusini na Pwani ya Kusini mvua zinatarajiwa kuwa juu hadi juu ya wastani isipokuwa Mkoa wa Lindi ambapo zitakuwa za wastani hadi chini ya wastani.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi  Mkuu  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr. Agnes Kijazi amesema kuwa hali ya malisho na maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori inatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi yanayopata mvua mara moja kwa mwaka.

Aliongeza kuwa katika maeneo  yale yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka hayatakuwa na ongezeko la maji na malisho na hivyo wafugaji wanashauriwa kutumia maji kwa uangalifu.

0 comments:

Post a Comment