Na Damas Makangale, MOblog kwa Msaada wa Mtandao
Hali ya bingwa wa zamani wa mbio za magari duniani Michael Schumacher imezidi kuimarika kidogo baada ya operesheni ya kupunguza maumivu na uvimbe kwenye shingo na ubongo wake, madaktari wake wamesema.
Madaktari walichukua vipimo vya (CT-Scan) mara moja ili kuweza kutambua ni wapi anavuja damu ndani ya ubongo wake na baada ya vipimo na matibabu hali yake imeonyesha ni bora zaidi walisema.
Bingwa huyo wa zamani wa mbio za magari aliyewika sana alipata majeraha makubwa sehemu ya kichwani siku ya Jumapili ya wili iliyopita katika nchi ya Ufaransa.
Familia yake ilichukua uamuzi mgumu wa kukubali operesheni ya ndugu yao na kutoa kibali kwa madaktari kuendelea na operesheni kwa muda wa saa mbili hivi.
” Hatuwezi kusema yeye alikuwa katika hatari kubwa sana lakini kwa sasa yupo imara na anapata nafuu kila baada ya muda kidogo , ” amesema Dk Jean- Francois

“Familia yote wana mengi sana wanataka kufahamu na kwamba hali yake bado ni nyeti na kitu chochote kinaweza kutokea .” amesema mmoja wa wanafamilia
Madaktari wamesema ilikuwa vigumu kutoa ubashiri kwa hali yake kwa kesho , muda wa miezi sita au hata wa mwaka.
Schumacher alikuwa kwenye spidi kali pamoja na mtoto wake mdogo gari ilipiduka na kugonga mwamba katika sehemu ya juu karibu na mji wa Moutiers nchini Ufaransa.
Prof Chabardes amesema dereva alikuwa katika “mbaya wakati analetwa katika hospitali ya mji wa moutiers na mishipa ya fahamu ilikuwa imeshuka kwa kasi na hajitambui.
Ujumbe wa msaada umekuja kutoka duniani kote.
Michael Schumacher alishinda michuano saba dunia wakati wa kazi yake ya mashindano ya magari
Msemaji wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kwa niaba ya Kansela wanatoa salamu za pole kwa Schumacher na familia yake na mamilioni ya wajerumani wanamuombea apone haraka.
0 comments:
Post a Comment