Fundi ‘Fataki” Abdul
Husein (31) mkazi wa Kijiweni Iringa akitoka mahakamani kupelekwa jela baada
ya kuhukumiwa na mahakama ya mwanzo bomani leo Huyu ndie mwanafunzi wa miaka 11 aliyeshinda vishawishi
vya fataki aliyefungwa jela jana
Binti huyo akiondoka
mahakamani hapo
Bw Abdul Husein akilia
baada ya kupewa haki yake ya kupenda wanafunzi
Ulinzi ukiwa umekamilika
nje na ndani ya mahakama
Safari ya fundi fataki
kwenda jela mwaka mmoja ikianzia hapa
----
FUNDI magari mkazi wa
kijiweni katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bw Abdul Husein (31)
amejikuta akitupwa jela mwaka mmoja na faini ya shilingi 200,000 baada
kutiwa hatiani na mahakama ya mwanzo bomani kwa kosa la kutaka penzi la
nguvu kwa mwanafunzi wa darasa la tano .
Fundi huyo ambaye anadaiwa
kukaribishwa katika nyumba hiyo kama mlinzi wa watoto wawili akiwemo
mwanafunzi huyo wa miaka 11 alitenda kosa hilotarehe 4 mwezi huu majira ya
saa 3 usiku baada ya kurejea kutoka katika shughuli
zake.
Akisoma hukumu hiyo leo
hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo bomani mheshimiwa Alois Masua alisema
kuwa katika ushahidi ambao ulitolewa mahakamani hapo na mtoto wa kiume wa
miaka 9 ulidai kuwa kijana huyo siku ya tukio baada ya kufika nyumbani
alimtaka binti huyo kumpa sahani ili aweke chips ambazo alikuja nazo
.
Kuwa baada ya binti huyo
jina limehifadhiwa na mtandao huu kumpa sahani ndani ya dakika chache
aliomba kupewa maji na binti huyo alifanya hivyo baada ya kupewa maji
kijana huyo alimtaka binti huyo kusogea kukaa katika eneo kochi ambalo
fundi huyo amekuwa akilitumia kama kitanda chake sebuleni kama mlizi bado
binti huyo aligoma kuingia majaribuni .
Hata hivyo haikuishia
hapo baada ya muda fundi huyo fataki alimtaka binti huyo kumsindikiza
chooni bado binti alionyesha msimamo wa kutamani masomo yake na kugoma
kumsindikiza kwa madai kuwa yeye ni binti na huyo ni mwanaume iweje aombe
kusindikizwa .
Kutokana na mbinu zote
kugonga mwamba ndipo fundi fataki huyo alipoamua kutumia njia ya mkato
ya kumkamata kwa nguvu binti huyo na kutaka kumbaka chooni kabla ya binti
huyo kuamua kupambana na kuishia kuchaniwa sketi yake .
Hali hiyo ilimfanya binti
huyo kutimua mbio na kuomba msaada kwa mama yake aliyekuwa amelala chumba cha
pili kabla ya mama mzazi na majirani kuamka na kumwadabisha fundi fataki
kwa kumpeleka polisi.
Hakimu Masua alisema kuwa
kutokana na ushahidi uliotolewa fundi huyo alipotakiwa kujitetea alikana
kujitetea kwa madai kuwa hawezi kuzungumza chochote katika mahakama
hiyo.
Hivyo alisema kutokana
na mtuhumiwa huyo kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza mahakama hiyo
ilipaswa kumfunga jela kwa miaka mitano kutokana na kosa hilo la shambulio
la aibu kifungu cha 135 kanuni ya adhabu namba 6 marejeo mwaka 2002
.
“ Mahakama hii inakuona
na hatia na hivyo inakupunguzia adhabu kutoka miaka mitano uliopaswa
kutumikia na kufungwa mwaka mmoja jela na ukitoka utatakiwa kumlipa
mlalamikaji kiasi cha Tsh 200,000”
0 comments:
Post a Comment