Sehemu ya dawa zilizokamatwa katka Operesheni.
Mkurugenzi
MKuu wa TFDA na DCI Manumba wakitazama sehemu ya dawa zilizokamaMamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) imekamata dawa bandia zenye thamani ya TSh. 49,634,733/= katika operesheni maalum ijulikanayo kamaOperesheni GIBOIAiliyoshirikisha Jeshi la Polisi nchini, Shirikisho la Polisi la Kimataifa (Interpol), Baraza la Famasi, TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Shirika la Viwango (TBS), Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Rais na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Operesheni GIBOIAilifanyika kuanzia tarehe 1-3 Oktoba, 2013 katika mikoa tisa ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma na Dar es Salaam.Operesheni hii pia imefanyika sanjari katika nchi saba zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo ni Afrika ya Kusini, Angola, Malawi, Msumbiji, Swaziland, Zambia na Tanzania kwa lengo la kupambana na dawa Bandia Barani Afrika. Wadau wa habari wakifuatilia maelezo kuhusu Operesheni GIBOIA.
Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini Kamishna Robert Manumba na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA katika mkutano na waandishi aw habari.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo akieleza waandishi kuhusu Operesheni GIBOIA.
Sehemu ya wadau wa Operesheni GIBOIA ktk mkutano.
DCI Manumba akitoa matokeo ya Operesheni GIBOIA kwa waandishi wa habari.
0 comments:
Post a Comment