Picha ya ramani ya kiwanda kitakavyokuwa ikikamilika kazi ya Ujenzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Meis Merey Ally Saleh akimpokea Dr Rashid aliyetembelea
kukagua kazi za ujenzi wa kiwanda cha saruji mjini Lindi.
Mhandisi
Rashid wa Sharjah alievaa kilemba akiangalia mchoro wa ujenzi alipokuwa
akikaua eneo la Ujenzi ambapo Mkurugenzi wa Meis na Meneja wake
wakitolea maelezo.
majengo na kazi inavyoendelea ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Na Abdulaziz Lindi
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Bandari ya Nchi ya Sharjah UAE, Mhandisi Rashid Al Leem
amefurahishwa na hatua ya Kampuni ya Meis kuanza kwa kasi ujenzi wa
kiwanda cha saruji katika wilaya ya Lindi huku akiutaka uongozi wa
kiwanda hicho kuongeza juhudi ili kukamilisha kwa wakati kama
ilivyokusudiwa ili mji huo uongeze ajira hali itakayosaidia kuinua
Uchumi.
Alibainisha
hayo alipokuwa akiongea na globu hii muda mfupi baada ya kukamilisha
ziara yake ya kukagua Ujenzi wa Kiwanda hicho alipokuwa kwenye ziara ya
kutembelea wilaya hiyo baada ya kukutana na Serikali ya Zanzibar ambapo
aliahidi Kuwekeza katika nyanja mbalimbali.
Dr
Rashid alisema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kuongeza kiwango
cha ajira, kipato cha wananchi wa kawaida wa mkoa wa Lindi na Taifa kwa
jumla na kupunguza gharama za ujenzi wa makazi kwa kupata saruji kwa bei
ya chini na kwa ukaribu kuliko ilivyo sasa.
“Kukamilika
kwa ujenzi wa kiwanda hiki itakuwa ni fursa ya pekee kwa wakazi wa
mikoa ya kusini kupata saruji kwa bei nafuu na ajira kwa vijana wa mikoa
hii ambapo Nchi yetu imeamua kutaka kuwekeza ndio maana pia
nitatembelea Bandari ya Mtwara.
Kwa
upande wake meneja wa mradi huo, Valerian Magembe alisema ujenzi wa
kiwanda hicho umefikia hatua mzuri kwani mitambo yenye thamani ya dola
za kimarekani milioni 25 kutoka nchini China inatarajiwa kuwasili hivi
karibuni baada ya kupakilwa huko shanghai,
“Mitambo
inayotarajia kuwasili ni mitambo mizito yenye cbm 6200 ya kusaga
mawe,kunyangia, kutenganisha, pamoja kuweka dawa,kuumua na kuunda
simenti na kwa sasa tayari imepakiwa kwenye meli toka Shaghahi, China na
ipo safarini itawasili muda wowote kuanzia sasa ”alisema Magembe.
Aliongeza
kuwa ujenzi wa kiwanda hicho uko kwenye hatua ya kusaga mawe baada ya
kufanya kazi kubwa ya kukata mlima ili kufanya eneo hilo liwe tambarale.
“Kazi
kwenye eneo ilikuwa ngumu kwani lina miinuko mikubwa hata hivyo sehemu
kubwa tumeikamilisha na tupo hatua za mwisho”alibainisha Magembe.
Aidha
ujezi wa kiwanda cha sementi Lindi ulinza mwezi februari mwaka 2013 na
unatarajia kukamilika septemba 214 na kuajiri watu zaidi 2000 pamoja na
kuzalisha tani 20000 kwa siku na kuongeza kipato kwa wakazi wa mkoa wa
Lindi.
Katika
ziara hiyo Dr Rashid aliongoza ujumbe toka Serikali ya Sharjah huku
akiwemo Balozi wa Comoro Nchini Balozi Islam Ally Saleh ambapo pia
msafara ulitembelea makazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
kimataifa,Bernard Membe kijijini Rondo wilayani humo
ANKAL MUHIDIN MICHUZI
ANKAL MUHIDIN MICHUZI
0 comments:
Post a Comment