SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, October 27, 2013

Mahafali ya kwanza ya shule ya WAMA-NAKAYAMA yafana Nyamisati Rufiji

1
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Salma Kikwete Mwenyekiti wa Taaisis ya Wanawake na Maendeleo WAMA wakati alipowasili katika viwanja vya mahafali katika mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari WAMA Nakayama yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani jana.Zaidi ya wanafunzi 60 walitunukiwa vyeti vya kumaliza kidato cha nne na zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wahitimu wakati wa mahafali hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na viongozi na watu mashuhuri akiwemo balozi wa Japan na wafanyabiashara ambapo mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi aliahidi kuisadia shule hiyo shilingi milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano mbazo ni kiasi cha shilingi bilioni moja kwa miaka hiyo mitano.
PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-NYAMISATI RUFIJI 1aa
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waaikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji. 2
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali wakati aliowasili shuleni hapo. 4
Watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo 5
Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la tukio kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya shule hiyo Dr. Ramadhan Dau. 5a
Wahitimu wakiingia katika eneo la tukio 6
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma kikwete akicheza na wanawake wenzake wake wa viongozi.
 6b
Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakiimba wimbo wa taifa uliooongozwa na wanafunzi wa shule ya WAMA Nakayama kutoka kulia ni Balozi anzania Mhe.Masaki Okada Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahiza, Mama Salma Kikwetena kutoka kushoto ni Dr. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa. 7
Baadhi wa walimu wa shule hiyo 7c
Baadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Daudi Nasibu katibu mkuu taaisis ya WAMA na Dan Kiondo. 8
Baadhi ya wananfunzi wa shule ya WAMA Nakayama 8c
Mh. Mbunge Vick Kamata akiongoza wanafunzi wa Wama Nakayama kuimba wimbo maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo.
99
Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa aakitoa historia ya shule hiyo 10g
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mjomba Band linaloongozwa na msanii Mrisho Mpoto akiigaiiza katika igizo maalum lililokuwa likitafsiri changamoto zinazomkabili mtoto wa kike yatima na anayeishi kwenye mazingira magumu katika suala zima la kupata elimu. 11
Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni Ndugu Jordan Lugimbana pamoja na waalikwa wengine katikati akiwa katika hafla hiyo 11h
Wahitimu wakiimba wimbo maalum wa kumshukuru Mwenyekiti wa WAMA mama Salma Kikwete 13Nyoka alikuwa ni moja ya burudani katika mahafali hayo 18
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Regnald Mengi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Aisha Bilal 19
Baadhi ya majengo ya shule hiyo. 20 21
Mdau Seraphin kutoka Serena Hotel alihudhuria pia 22
Mama Salma Kikwete katikati akiimbiwa wimbo maalum na wahitimu 23
Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete akicheza wimbo maalum ulioimbwa na wanafuzni wahitimu katika mahafali hayo 24
27 28 29
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na makundi mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mahafli hayo jana

0 comments:

Post a Comment