SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, October 10, 2013

Kenya:Hakuna rais amewahi kufika ICC

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed (Pichani) amesema kuwa hakuna rais hata mmoja aliye madarakani amewahi kufikishwa mbele ya mahakama ya ICC.


Taarifa hii bila shaka imetafsiriwa na wengi kuwa mpango wa Kenya kutokubali Rais Uhuru Kenyatta kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC mwezi ujao.

Duru zinasema kuwa hofu kuwa huenda Kenyatta akakosa kufika mahakamani kama alivyoamrishwa na mahakama.

Waziri Amina amesema kuwa Rais Kenyatta yuko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC lakini kwa kuwa yeye ni rais hali imebadilika.

Kenyatta anatakiwa na mahakama ya ICC kuhusiana na uhalifu dhidi ya binadamu katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007/2008

Bi Abdalla amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.

Wakati huohuo, Kenya imekanusha madai kuwa inashinikiza mataifa mbalimbali ya Afrika kujiondoa katika mkataba wa Roma uliobuni mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC.

Waziri wa mashauri ya kigeni nchini humo Balozi Amina Mohamed kuwa Kenya imekuwa ikishirikiana na mahakama hiyo na hata Naibu wa Rais William Ruto kwa sasa yuko mjini the Hague kuhudhuria vikao vya mahakama hiyo.

Matamshi ya Bi Amina yanakuja siku chache tu kabla ya mkutano wa Marais wa Afrika utakaofanyika Ethiopia jumamosi hii.

Bi Amina amesema kuwa Kenya haijashinikiza nchi yoyote kuondoka kwenye mkataba wa Roma na kuwa mkutano wa AU umeitishwa na nchi tofauti wala sio Kenya.

Kadhalika Amina amesema kuwa Kenya haina nia yoyote ya kutoendelea kushirikiana na mahakama ya ICC.

Wakati huohuo mwanasheria mkuu wa Kenya Githu Muigai amepewa fursa ya kuielezea mahakama ya ICC kwa nini bunge la Kenya lilipitisha hoja ya kuitaka Kenya kujiondoa kutoka katika mkataba wa Roma.

Majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto, wamesema kuwa maelezo ya Muigai yatasaidia mahakama kuchukua hatua zaidi za kuwalinda mashahidi ambao tayari wametoa ushahidi wao.

Jaji mkuu anayeongoza jopo la majaji wanaosikiliza kesi dhidi ya Ruto, Chile Eboe-Osuji,ambaye alieleza kuwa wanajadili swala hilo na kuwa maelezo ya Muigai kuhusu mkakati wa serikali kutaka kuiondoa Kenya kutoka katika mahakama ya ICC utawasaidia kufanya uamuzi. BBC 

0 comments:

Post a Comment