Gari
Maalum lililobeba Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah (Uncle
J),likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es
Salaam tayari kwa zoezi la kuaga Mwili huo ambao utasafirishwa kwenda
Kijijini kwao Tarime,mkoani Mara kwa Mazishi.Marehemu Julius Nyaisangah
alikuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One,
akitokea Radio Tanzania (RTD) yeye pamoja na Mikidadi Mahmoud mwanzoni
mwa miaka ya 90.
Waanzilishi wengine ni Aboubakary Liongo, Rankim Ramadhan, Flora
Nducha,Vicky Msina,Taji Liundi,Charles Hillary na Blandina
Munghezi.Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma
Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha
mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji
wengine.
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbali mbali hapa nchini wakishirikiana kwa
pamoja kubeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah (Uncle J)
ulipowasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam leo.
Mmoja
wa Wanahabari waliowahi kufanya kazi na Marehemu Julius Nyaisangah,Dkt.
Misanya Bingi akiwa amebeba msalaba wenye jina la Marehemu.
Mwili ukihifadhiwa sehemu iliyoandaliwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu
Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa
Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD).Marehemu Nyaisangah
atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na
vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya
Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akiwasili kwenye Viwanja vya
Leaders Club,jijini Dar es Salaam leo kushiriki Kuaga Mwili wa Marehemu
Julius Nyaisangah.Wanaompokea na Wajumbe wa Kamati ya Mazishi (kushoto)
ni Aboubakar Liongo na kulia ni Teddy Mapunda.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi
wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam
kuungana na Waombolezaji wengine kuaga Mwili wa Marehemu Julius
Nyaisangah.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Mazishi ya Marehemu Julius
Nyaisangah pamoja na Waombolezaji mbali mbali,wakati alipowasili
viwanjani hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akiwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya
Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe pia yupo Viwanjani hapa kushirikiana
na Waombolezaji mbali mbali kuaga mwili wa Marehemu Julius
Nyaisangah.Kushoto ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania,Haidan
Ricco.
Wadau
mbali mbali wapo viwanjani hapa,Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni
ya New Habari,Absaloum Kibanda na katikati ni Muimbaji wa Muziki wa
Dansi wa siku nyingi,Mzee Hassan Bichuka.
Waombolezaji.
Wasifu wa Marehemu ukisomwa na Bw. Mapunda.
Wanahabari wakichukua tukio zima la Kuaga.
Wadau mbali mbali wakiwemo waliowahi kufanya kazi na Marehemu,wakishiriki msiba huo.
Mtangazaji Mkonge nchini,Masoud Masoud akiongoza taratibu za Kuaga.
NA MICHUZI MATUKIO BLOG
0 comments:
Post a Comment