SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, September 19, 2013

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTOAJI LESENI ZA BIASHARA CHINI YA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA. 25 YA 1972 KWA MFUMO WA KUHUISHA NA KULIPIA ADA

 Afisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Nicodemus Mushi (kushoto) akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu utoaji leseni za biashara chini ya sheria ya leseni za Biashara Na. 25 ya 1972 kwa Mfumo wa Kuhuisha na Kulipa ada,wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.
 Afisa Biashara Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Christopher Nassari (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mfumo huo wa ulipaji ada na kuwataka wafanyabiashara kulipa ada hizo mapema kabla ya tarehe 31 Desemba 2013 ili kuepuka adhabu na faini, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Habari na Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw.Nicodemus Mushi
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo.Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
 ---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 

1.   UTANGULIZI 
Serikali ilirudisha rasmi utozaji wa ada za Leseni za biashara kupitia Sheria ya Fedha Na.5 ya mwaka 2011. Maandalizi yamekuwa yakifanyika kutoka wakati huo na ada zimeanza kutozwa rasmi 01/07/2013 kwa mfumo wa kuhuishwa (Renewal).

Kutokana na marekebisho hayo, utaratibu wa kutoa Leseni za Biashara BILA MALIPO uliondolewa na kusitishwa na Serikali tarehe 30 Juni, 2013. Leseni za Biashara zilizotolewa kuanzia tarehe 1 Julai, 2004 hadi  30 Juni, 2013 ambazo hazikuwa na UKOMO zinatakiwa kupelekwa kwenye Mamlaka zilizotoa Leseni hizo, ili zihuishwe na kulipiwa  ada kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa Serikali.

Kila mfanyabishara mwenye Leseni ya Biashara anapaswa kujaza Fomu ya Maombi ya Leseni  ya Biashara na kuambatisha Leseni ya Biashara aliyonayo na kuiwasilisha katika Mamlaka husika, kwa ajili ya kuhuisha na  kulipia ada. Maombi yapelekwe katika Mamlaka iliyotoa Leseni husika. Kwa Leseni za Biashara za kundi “A” kama ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya Leseni  ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara. Maombi hayo  yawasilishwe katika Ofisi za  Wizara ya Viwanda na Biashara zilizopo Barabara ya Sokoine  Jengo la NSSF-“Water front”, Ghorofa ya Nne chumba Na. 416. Kwa wale Wafanyabiashara wa Kundi “B” kama ilivyoainishwa kwenye Fomu ya Maombi ya Leseni  ya Biashara TFN Na. 211ya 2004 wafike Ofisi za Halmashauri za Majiji,  Manispaa na Wilaya zilizo katika maeneo yao, watapata huduma kutoka kwa Maafisa Biashara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.


2.   UTARATIBU WA KUFUATA ILI KUFANIKISHA ZOEZI NA KUPATA HUDUMA KWA HARAKA 

  1. Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wajaze Fomu ya Maombi ya Leseni za Biashara (fomu inapatikana katika tovuti ya Wizara sehemu ya Marketing Sector (www.mit.go.tz) au fika Wizarani NSSF-Waterfront ghorofa ya 4 chumba Na. 416, Kwa Wafanyabiashara wa Kundi “B” wawasilishe  maombi Ofisi za Halmashauri za Majiji,  Manispaa na Wilaya zilizo katika maeneo yao;
  2. Waambatishe Leseni za Biashara za kudumu walizonazo na kuwasilisha kwenye Mamlaka husika kama ilivyoainishwa hapo juu;
  3. Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wafanye malipo kupitia Benki ya CRDB mahali popote kwa kutumia Account Number 0150413356300; jina Revenue Collection Trading License-MIT. Wafanyabiashara wa Kundi “B” wataelekezwa Benki ya kulipia na Halmashauri zao;
  4. Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wawasilishe “pay slip” ya Benki ghorofa ya Mezanine (NSSF-WaterFront) kwaajili ya risiti ya Serikali, Wafanyabiashara wa Kundi “B” wataelekezwa Ofisi ya kuwasilisha ili wapewe reisiti ya Serikali-Mweka Hazina wa Halmashauri;
  5.  Kwa wafanyabiashara wa Kundi “A” wawasilishe Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara, Leseni ya Biashara na  risiti ya malipo ghorofa ya 4 kwa ajili ya kuandikiwa Leseni ya Biashara, Wafanyabiashara wa Kundi “B” wataelekezwa ofisi ya kupeleka na kuandikiwa Leseni ya Biashara ofisi za Biashara za Halmashauri.
Waombaji wapya wa Leseni za Biashara  mnapaswa kujaza fomu ya maombi ya Leseni za Biashara na kuambatisha nyaraka kama inavyojieleza katika fomu ya maombi na kufuata hatua ya 1 hadi 5 kama ilivyoelezwa hapo juu.
Mnashauriwa kuhuisha na kulipia ada Leseni za Biashara mapema kabla ya tarehe 31 Desemba, 2013 ambapo  adhabu na faini kwa wafanyabiashra watakaochelewa kuhuisha (Renew)  itaanza kutolewa tarehe 1 Januari, 2014.


  1. TAHADHARI
 Wafanyabiashara mnatadharishwa kuwa hapa mjini kuna mawakala wasio waaminifu maarufu kwa jina la VISHOKA. Mnashauriwa kuwaepuka na muweke utaratibu wa kufuatilia Leseni za Biashara zenu wenyewe.
Kwa wale ambao, wameshaletewa Leseni za Biashara na mawakala waliowatuma mnashauriwa kwenda kwenye Mamlaka iliyotoa Leseni husika kwa ajili ya kufanya uhakiki kwa kuwa imebainika kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya biashara kwa kutumia Leseni batili (Feki) 
TAFADHALI FIKA NA KUFANYA UHAKIKI KWA FAIDA YA BIASHARA YAKO.

MAELEZO ZAIDI YANAWEZA KUPATIKANA PIA KWA KUTUMIA ANUANI IFUATAYO:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Viwanda na Biashara,
S. L. P. 9503,
Simu Na-+255-22-2127897/8,
Fax: +255-22-2125832
Website – www.psmit.go.tz
DAR ES SALAAM.
WIZARA YAVIWANDA NA BIASHARA 

0 comments:

Post a Comment