SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, September 19, 2013

Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Amwapisha Msham Abdula Khamis kuwa Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Zanzibar

 Makamu wa kwanza wa Rais Maalim  Seif Sharif Hamad,akisalimiana na Viongozi wakati alipohudhuria katika ukumbi wa Ikulu  Mjini Unguja, wakati wa  hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto,Msham Abdula Khamis,leo asubuhi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Msham Abdula Khamis kuwa Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Unguja jana asubuhi.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora,Dk.Mwinyihaji Makame,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto,Msham Abdula Khamis,jana asubuhi.
Mawaziri wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu  Mjini Unguja, wakati wa  hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto,Msham Abdula Khamis,jana asubuhi.
Picha na Ramadhan Othman,IKULU-Zanzibar

0 comments:

Post a Comment