SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, September 9, 2013

CHAMA CHA WASANII JIJI LA MBEYA CHAPATA VIONGOZI BAADA YA KUFUFUA UMOJA WAO.

Afisa Utamaduni wa Jiji, Nimwindael Mjema akizungumza na wasanii hao kabla ya kuanza uchaguzi
 Afisa kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi, Julius Mwambogela akiongea na wasanii wa mkoa wa Mbeya.
Huyu ndiye Mwenyekti mpya wa Chama cha wasanii mkoa wa Mbeya Samweli Mwamboma====
Chama cha wasanii Jiji la Mbeya kimefufua umoja wao na hatimaye kufanya uchaguzi kupata viongozi watakaowaongoza kwakipindi cha miaka mitatu katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Coffee Garden Jijini Mbeya na kusimamiwa na Viongozi wa Jiji la Mbeya akiwemo Afisa kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi, Julius Mwambogela na Afisa Utamaduni wa Jiji Nimwindael Mjema. 
Wasanii wa Chama cha Wasanii Jiji la Mbeya ambao wamefufua umoja wao baada ya kukaa muda mrefu bila kushikamana licha ya usajili kufanyika Mwaka 2004 ambapo wametakiwa kufuata malengo yaliyowafanya wajiunge na umoja huo.
Katika uchaguzi huo jumla ya nafasi Sita zilichaguliwa zikiwa za Wajumbe Wanne, Mtuza hazina, Katibu Msaidizi, Katibu, Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti ambao walichaguliwa kutoka kwa wapiga kuru 30 kutoka vikundi 10 vya sanaa ndani ya jiji la Mbeya waliowakilishwa na wajumbe watatu kila kundi.
Makundi ya sanaa yaliyowakilishwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Tupume, Bantu,Volcano, Kasi Mpya, Sombe, Umbe, UWT Isanga, Sisi family, Isika, Golden Power na Umoja.
Hata hivyo uchaguzi huo ulifanyika kwa utulivu mkubwa huku nafasi za wajumbe zikiwa na wagombea wanne ambao wote walipitishwa kutokana na katiba yao kuruhusu wajumbe wenye idadi hiyo lakini ikihitaji kupitishwa kwa zaidi ya nusu ya kura.
Akitanaza matokeo ya uchaguzi huo Afisa Utamaduni wa Jiji, Nimwindael Mjema alisema Wajumbe waliopitishwa ambao kura zao zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Chihanga Timotheo (20), Clemence Dachi(15), Kenny lunguya (25) na rajabu mrisho Rajabu (20).
Alimtangaza aliyeshinda nafasi ya utunza hazina kuwa ni Peter Mwambala aliyepata kura za ndiyo 21 na kur za hapana 8 baada ya mgombea pekee wa nafasi hiyohuku nafasi ya Katibu Msaidizi ikinyakuliwa na Bahati Shulula baada ya kmbwaga mpinzani wake Shabani Lazack kwa kura  27 dhidi ya 2.
Alisema nafasi ya Katibu wa Chama hicho cha wasanii Jiji la Mbeya imechukuliwa na Ramadhani Shabani baada ya kura 23 dhidi ya Peter Anton aliyepata kura 5, na nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikiwa na mgombea mmoja ambaye ni Halima Ntandu aliyepitishwa kwa kura za ndiyo 28 huku kura mbili zikimkataa.
Nafasi ya Mwenyekiti ilichukuliwa na Samweli John Mwamboma aliyepita kwa kishindo baada ya kupata kura 29 dhidi ya mpinzani wake Zwadi Mtavangu aliyejinyakulia kura Moja pekee kutoka kwa wapiga kura waliojitokeza.

Na Mbeya yetu

0 comments:

Post a Comment