Mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga akiongea wakati wa
uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia ada za
leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money pichani kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana
Masalla (kulia) Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel
Adriana Lyamba.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs.Diana Masalla
(wa pili kushoto) akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani,
DCP Mohamed Mpinga na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel
Adriana Lyamba kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa
Airtel kulipia ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money
wakishuhudia kulia ni meneja kitengo cha Airtel money John Ndunguru ,
mwisho kushoto ni mwakilishi wa max malipo Tumsifu Lema.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs.Diana Masalla
(wa pili kushoto) akifatiwa na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani,
kwa pamoja wakizindua huduma itakayowawezesha wateja wa Airtel kulipia
ada za leseni ya magari kupitia huduma ya Airtel money.
Airtel
Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania TRA wamezindua
rasmi huduma ya kufanya malipo ya ada za leseni za magari kupitia huduma
ya Airtel money. Huduma hii inapatikana bure kwa wateja wote wa Airtel
nchi nzima. Hii inawawezesha watumiaji wa huduma hii kulipia leseni ya
magari yao wakiwa ofisini au majumbani mwao kwa urahisi zaidi ambapo kwa
sasa ni BURE.
Adriana
Lyamba, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel amesema "
huduma ya kulipia leseni ya magari kupitia Airtel money imeleta unafuu
kwa wateja watakaotaka kulipia leseni za magari. Huu ni mwendelezo wa
mapinduzi ya huduma za kifedha kupitia huduma ya Airtel money
inayomuhakikishia mteja uharaka, unafuu, usalama na urahisi zaidi katika
kulipia huduma mbalimbali. Tunaamini huduma hii ya kulipia leseni za
magari kupitia Airtel money kutaleta ufanisi na kuendeleza juhudi za
serikali katika ukusanyaji wa kodi.
Tunaahidi
kuendelea kuleta suluhisho katika huduma za malipo mbalimbali na
kuwahakikishia wateja wetu urahisi, usalama na ufanisi zaidi kupitia
Airtel Money."
Sasa
tumewawezesha wateja wote wa Airtel kulipia leseni za magari bila kuwa
na haja ya kutembelea ofisi za TRA kufanya malipo. Wateja watatakiwa
kwenda kuchukua leseni/stika zao pale malipo yatakapofanyika na
leseni/stika zao kuwa tayari.
Akiongea
kuhusu huduma ya malipo ya ada za leseni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo
cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Mrs. Diana Masalla alisema" huduma hii
mpya inahusisha malipo ya ada za lesseni za magari, ada za uamisho wa
magari pamoja na malipo mengine ya ada za usajili wa magari. Huduma hii
itawezesha ukusanyaji wa malipo ya ada / kodi zifanyike kwa njia rahisi
na nafuu. Unaweza kupata kiasi cha kulipia ada unayotakiwa kulipia kisha
ukalipia hapohapo ndani ya sekunde chache kupitia huduma ya Airtel
money.
Ulipaji
huu unaenda sambamba na kauli mbiu ya TRA ya Urahisi, Uhiari na
Uboreshaji Endelevu Akiongea juu ya namna ya ulipiaji ada Meneja wa
kitengo cha Airtel money John Ndunguru alisema" huduma hii inapatikana
kwa wateja wa malipo ya awali na ya mwenzi.
Aliongeza
kwa kusema ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hii, Airtel imeweza
kuiweka kwenye MENU ya Airtel Money "TRAMAGARI" ili kuweza kurahisisha
ulipaji wa ada na kuiwezesa serikali kukusanya ada kwa gharama nafuu
zaidi".
Kwa
upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga
alisema "Ninawapongeza sana kampuni ya Airtel Kupitia huduma yake ya
Airtel Money kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
kurahisisha ukusanyaji wa kodi hii ya Ada za magari maarufu kama Road
License. Hi ni huduma nzuri inayosaidia watanzania kuokoa muda wao pale
wanapoweza kutumia simu zao kupitia mtandao wa Airtel kulipia Ada ya
magari yao kila mwaka bila usumbufu."
Kwa
urahisi huu inatusaidia sana kuokoa muda ambao ungepotea kukaa kwenye
foleni ya malipo na badala yake muda tunaookoa tutautumia katika
shughuli nyingine za kiuchumi.
Naomba
niwakumbushe kuwa wiki ya usalama barabarani itaanza wiki ijayo tarehe
23.9.2013 hivyo mambo yote ya ukaguzi wa stika za ada za magari yaani
(Road Licence) pamoja na Stika za usalama barabarani na ukaguzi wa
vyombo vyote vya moto utaenda sambamba, hivyo ninawakumbusha watumiaji
wote wa vyombo vyote vya moto kufuata sheria zote zilizowekwa ili
kuepuka adhabu ya kulipa faini.
Huduma
ya Airtel money inawawezesha wateja kutumia simu zao za mkononi katika
huduma za kifedha zikiwemo kulipa bill ya maji DAWASCO, kulipia Luku
TANESCO malipo ya DSTV, kulipia visa ya USA na sasa ada za lesseni ya
magari. Airtel money ni huduma rahisi na salama inayotoa huduma za
mobile benki na za malipo mbalimbali.




0 comments:
Post a Comment